• HABARI MPYA

    Wednesday, November 20, 2013

    BAFANA BAFANA YAWACHAPA KIDUDE HISPANIA FNB

    Na Naseem Mahmoud, Joannesburg
    AFRIKA Kusini imewafunga mabingwa wa dunia, Hispania 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa jana usiku Uwanja wa FNB.
    Shukrani kwake, Bernard Parker (pichani chini) aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 10 ya kipindi cha pili, Bafana ikijifariji kwa kukosa tiketi ya Kombe la Dunia.

    Hispania ilitawala robo ya kwanza ya mchezo, lakini ikashindwa kufunga mabao. Mshambuliaji David Villa alitumbukiza mipira miwili nyavuni, lakini yote marefa wakasema alikuwa ameotea.
    Bafana Bafana ilikaribia kupata dakika ya 18 kupitia kwa Oupa Manyisa aliyepga shuti lililogonga mwamba, huku kipa Iker Casillas akibaki kaduwaa.
    Mshambuliaji wa Juventus, Fernando Llorente aliruka peke yake kupiga kichwa dakika ya 27 kufuatia makosa ya beki ya Bongani Khumalo, lakini bahati nzuri akapaisha akiwa amebaki na Itumeleng Khune.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BAFANA BAFANA YAWACHAPA KIDUDE HISPANIA FNB Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top