• HABARI MPYA

    Wednesday, November 20, 2013

    ROBINHO AIPIKU REKODI YA PELE BRAZIL IKIIUA CHILE 2-1

    MSHAMBULIAJI Robinho (pichani) alitokea benchi na kuifungia bao la ushindi Brazil ikishinda 2-1 dhidi ya Chile jana, akifikisha mabao tisa aliyowafunga yeye peke yake wapinzani wao hao wa Amerika Kusini.
    Robinho, ambaye sasa amefunga bao zaidi ya Pele dhidi ya Chile, aliitwa te kikosini mwezi huu kwa ajili ya mechi za kirafiki dhidi ya Chile na Honduras baada ya miaka miwili ya kuwekwa nje.
    Brazil inatarajiwa kucheza mechi moja zaidi ya krafiki dhidi ya Afrika Kusini mjini Johannesburg Machi mwakani, kabla ya Scolari kutangaza kikosi chake cha Kombe la Dunia.
    Brazil wanaandaa fainali za mwakani za Kombe la Dunia, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza tangu 1950.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ROBINHO AIPIKU REKODI YA PELE BRAZIL IKIIUA CHILE 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top