• HABARI MPYA

    Wednesday, November 20, 2013

    UHOLANZI YAMALIZA MWAKA BILA KUFUNGWA...

    UHOLANZI imemaliza mwaka bila kufungwa hata mechi moja baada ya sare ya bila kufungana na Colombia katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa jana mjini Amsterdam.
    Uholanzi ililazimika kucheza na wachezaji 10 kwa kiasi cha saa moja baada ya Jeremain Lens kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 35, wakati pia iliwapoteza Siem de Jong na Rafael van der Vaart walioumia kabla ya mapumziko.
    Walipata nafasi nzuri ya kufunga mapema kwenye mchezo huo, lakini van der Vaart akagongesha mwamba. Uholanzi ambayo ilitoka sare ya 2-2 na Japan Jumamosi, imeshinda mechi saba na sare tano katika mechi zake 12 za mwaka 2013.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UHOLANZI YAMALIZA MWAKA BILA KUFUNGWA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top