• HABARI MPYA

    Monday, December 02, 2013

    WACHEZAJI WAWILI ERITREA WATOWEKA NAIROBI KAMA KAWA

    Na Zaituni Kibwana, Nairobi
    WACHEZAJI wawili wa Eritrea wameripotiwa kutoroka wakati wakijiandaa na mchezo wa leo wa Kundi C, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge dhidi ya Uganda.
    Ofisa wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) anayewaongoza Eritrea mjini hapa, Albert Shamola amesema kwamba wachezaji hao hawakuonekana baada ya kurejea kutoka uwanjani kuangalia mechi za jana.
    Hii si mara ya kwanza kwa wachezaji wa Eritrea kutorokea nchi za watu wanapokwenda kwenye mashindano, kwani wamekwishawahi kufanya hivyo Tanzania pia mwaka 2010 na Uganda mwaka jana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WACHEZAJI WAWILI ERITREA WATOWEKA NAIROBI KAMA KAWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top