• HABARI MPYA

    Friday, January 10, 2014

    ANCELOTTI AMFANYIA 'ROHO MBAYA' WENGER, AMKAZIA MACHO NA KUMUWEKEA 'KIBESI' MCHANA KWEUPEE; "MORATA HAENDI POPOTE"

    KOCHA wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesistiza mchezaji anayetakiwa na Arsenal, Alvaro Morata hatakwenda popote Januari baada ya kupewa dakika 10 za kucheza kaika ushindi wa 2-0 dhidi ya Osasuna jana kwenye Kombe la Mfalme.
    Mshambuliaji mwenzake, Jese Rodriguez aliifungia bao la pili Real, na kinda huyo ni moja  sababu za Arsenal kuamini wanaweza kumpata kwa mkopo Morata kutoka Bernabeu.
    "Hatujabadilisha mtazamo wetu hata kidogo" amesema Ancelotti baada ya ushindi. "Morata anabaki hapa na hajatuambia sisi kama anataka kuondoka,".
    Haendi popote: Carlo Ancelotti amesema Alvaro Morata anabaki Real Madrid
    Win: The Real Madrid boss saw his side beat Osasuna 2-0 in the first leg of the Copa del Rey last 16
    Ushindi: Kocha wa Real Madrid aliishuhudia timu yake ikiichapa Osasuna 2-0 katika mechi ya kwanza ya 16 Bora Kombe la Mfalme jana

    Arsene Wenger amesema yuko sokoni kutafuta mshambuliaji kufuatia Theo Walcott kupata maumivu makubwa ya goti na Morata yupo juu katika orodha ya wachezaji anaowawania.
    Olivier Giroud anatarajiwa kurejea kikosini Arsenal kuelekea mchezo na Aston Villa Jumatatu, lakini bado Wenger anasema hana washambuliaji wa kutosha.
    Kuimarika tena kwa Lukas Podolski angalau kutampa ahueni Wenger, wakati Alex Oxlade-Chamberlain naye akipata ahueni taratibu, lakini kama Arsenal itapoteza mchezaji mmoja au wawili zaidi, itawagharimu mwishoni mwa msimu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ANCELOTTI AMFANYIA 'ROHO MBAYA' WENGER, AMKAZIA MACHO NA KUMUWEKEA 'KIBESI' MCHANA KWEUPEE; "MORATA HAENDI POPOTE" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top