TIMU ya Arsenal itaongeza juhudi katika kuhakikisha inamsajili kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata wiki hii.
Kuumia goti kwa Theo Walcott wakati ambao tayari Nicklas Bendtner ana matatizo ya muda mrefu ya kifundo cha mguu kunamfanya kocha Arsene Wenger alazimike kusajili mshambuliaji mpya wa kati mwezi huu.
Anatakiwa kwa mkopo: Arsenal inataka kumsajili kwa muda mshambuliaji Real Madrid, Alvaro Morata, pichani akishangilia baada ya kufunga bao dhidi ya Levante Oktoba mwaka jana
Wenger anaona Morata ni mtu sahihi kuziba pengo katika timu yake kuanzia sasa hadi mwishoni mwa msimu, lakini Real imewaambia The Gunners kinda huyo mwenye kipaji hawezi kuuzwa moja kwa moja, bali kutolewa kwa muda mfupi inawezekana



.png)
0 comments:
Post a Comment