• HABARI MPYA

    Wednesday, January 08, 2014

    AZAM TV KUWAGAWIA VING’AMUZI WACHEZAJI KOMBE LA MAPINDUZI

    Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
    KAMPUNI ya Azam Media Group itatoa zawadi ya king’amuzi kwa mchezaji bora wa kila mechi kuanzia hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayoendelea visiwani Zanzibar.
    Robo Fainali zote zinachezwa leo kwenye viwanja viwili, Gombani, Pemba na Amaan, Zanzibar.
    Kwenye Uwanja Gombani, mabingwa watetezi Azam FC watamenyana na Cloves Stars Saa 10:00 jioni, mechi itakayotanguliwa na mchezo mwingine wa hatua hiyo kati ya KMKM na URA ya Uganda.
    Nahodha wa KMKM, Ali Khamis alipata zawadi ya king'amuzi cha Azam TV kwa kufunga bao kwanza Uwanja wa Amaan katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Mapinduzi mwaka huu. Hapa anakabidhiwa king'amuzi hicho na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Geoffrey Nyange 'Kaburu'.

    Uwanja wa Amaan, Zanzibar mabingwa wa zamani wa michuano hiyo, Simba SC watamenyana na Chuoni ya Pemba kuanzia Saa 2:00 usiku, mechi itakayotangulia na mchezo mwingine kati ya KCC ya Uganda na Tusker ya Kenya. 
    Mgeni rasmi katika mchezo wa leo usiku Uwanja wa Amaan, anatarajiwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, ambaye ataongozana na Mjumbe wa Kamati yake ya Utendaji, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’.
    Washindi wa mechi za leo watamenyana keshokutwa kusaka timu za kuingia Fainali Uwanja wa Amaan, wakati Fainali ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu itachezwa Januari 13 Uwanja wa Amaan.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM TV KUWAGAWIA VING’AMUZI WACHEZAJI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top