• HABARI MPYA

    Wednesday, January 08, 2014

    YANGA SC WANAONDOKA ALFAJIRI YA KESHO KWENDA UTURUKI KWA KAMBI YA WIKI MBILI

    Na Prince Akbar, Dar es Salaam
    MSAFARA wa zaidi ya watu 32 wa Yanga SC unatarajiwa kuondoka kesho alfajiri kwenda Uturuki kwa kambi ya wiki mbili, kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Yanga wanatarajiwa kupata viza zao jioni ya leo na kesho watapanda ndege ya Uturuki (Turkish Airline) kwenda kwenye kambi ya mafunzo katika nchi hiyo ya Ulaya kwa mara ya pili mfululizo.  

    Matunda ya Uturuki: Yanga SC ilitwaa ubingwa mwaka jana baada ya ziara ya Uturuki, je na mwaka huu itakuwa na manufaa?

    MSAFARA WA YANGA SC UTURUKI:

    1. Juma Kaseja
    2. Deo Munishi ‘Dida’
    3. Ally Mustafa ‘Barthez’
    4. David Luhende
    5. Oscar Joshua
    6. Juma Abdul
    7. Mbuyu Twite
    8. Nadir Haroub ‘Cannavaro’
    9. Kevin Yondan
    10. Job Ibrahim
    11. Rajab Zahir
    12. Hassan Dilunga
    13. Frank Domayo
    14. Hamisi Thabit
    15. Bakari Masoud
    16. Haruna Niyonzima
    17. Nizar Khalfan
    18. Jerry Tegete
    19. Hamisi Kiiza
    20. Emmanuel Okwi
    21. Mrisho Ngassa
    22. Said Bahanuzi
    23. Shaaban Kondo
    24. Didier Kavumbangu
    25. Simon Msuva
    26. Reliant Lusajo
    27. Hussein Javu
    28. Charles Boniface Mkwasa (Kocha)
    29. Juma Pondamali (Kocha)
    30. Juma Sufiani (Kocha)
    31. Hafidh Saleh (Meneja)
    32. Baraka Kizuguto (Ofisa Habari).
    Wachezaji wanaotarajiwa kuondoka na timu hiyo kesho ni makipa; Juma Kaseja, Deo Munishi ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki David Luhende, Oscar Joshua, Juma Abdul, Mbuyu Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Job Ibrahim na Rajab Zahir.
    Viungo ni Hassan Dilunga, Bakari Masoud, Hamisi Thabit, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, wakati washambuliaji ni Jerry Tegete, Hamisi Kiiza, Emmanuel Okwi, Mrisho Ngassa, Said Bahanuzi, Shaaban Kondo, Didier Kavumbangu, Simon Msuva, Reliant Lusajo na Hussein Javu.
    Viongozi ni makocha Charles Boniface Mkwasa na Juma Pondamali, Daktari Juma Sufiani, Meneja Hafidh Saleh na Ofisa Habari, Baraka Kizuguto. 
    Kunaweza kukawa na watu wengine katika msafara huo kutoka kwenye uongozi, lakini bado haijajulikana ni akina nani.
    Wachezaji ambao wameachwa ni Athumani Iddi ‘Chuji’ aliyesimamishwa kwa utovu wa nidhamu, Salum Abdul Telela ambaye ni majeruhi na wachezaji waliopandishwa kutoka timu ya vijana, Issa Ngao, Yussuf Abdul na Abdallah Mguhi ‘Messi’.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WANAONDOKA ALFAJIRI YA KESHO KWENDA UTURUKI KWA KAMBI YA WIKI MBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top