• HABARI MPYA

    Monday, January 06, 2014

    AZAM WAIFANYIA ‘ROHO MBAYA’ ASHANTI MAPINDUZI, WAICHAPA KIDUDE NA KUIPANDISHA BOTI KUREJEA ILALA

    Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
    HATUA ya makundi ya Kombe la Mapinduzi imehitimishwa usiku huu kwa mchezo wa mwisho wa Kundi C, Azam FC ikiilaza Ashanti United bao 1-0 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
    Bao pekee la Azam leo limefungwa na Mganda, Brian Umony dakika ya 60, akiunganisha krosi ya Kipre Tchetche kutoka wingi ya kulia.
    Kipre Tchetche akimpongeza Brian Umony baada ya kufunga leo Uwanja wa Amaan

    Kwa matokeo hayo, Ashanti inayofundishwa na kocha mkongwe, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ inaaga mashindano haya. Ashanti ilihitaji sare tu katika mchezo wa leo ili ifuzu Robo Fainali, lakini imalambwa kidude.  
    Timu zilizofanikiwa kuingia Robo Fainali ni Azam FC na Tusker ya Kenya kutoka Kundi C, Simba SC na KCC ya Uganda kutoka Kundi B, URA ya Uganda, Chuoni, Cloves Stars na KMKM.
    Robo Fainali zitachezwa Jumatano, Tusker na URA Saa 8:00 mchana na Azam FC na Cloves Saa 10:00 jioni Uwanja wa Gombani Pemba na Uwanja wa Amaan, mechi ya kwanza itakuwa kati ya KCC na KMKM Saa 10:00 na Simba SC na Chuoni Saa 2:00 Usiku.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM WAIFANYIA ‘ROHO MBAYA’ ASHANTI MAPINDUZI, WAICHAPA KIDUDE NA KUIPANDISHA BOTI KUREJEA ILALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top