• HABARI MPYA

    Monday, January 06, 2014

    'UCHAWI' WA MBEYA CITY HAUVUKI BAHARI, YATOLEWA MAPEMA KOMBE LA MAPINDUZI

    Na Mwajuma Juma, Zanzibar
    MBEYA City imefungishwa virago Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, baada ya kufungwa bao 1-0 na URA ya Uganda Uwanja wa Gombani, Pemba jioni ya leo.
    Kwa matokeo hayo, Mbeya City inaaga mashindano hayo kwa pointi yake moja iliyovuna kutokana na sare na Clove Stars, huku URA ikiungana na Chuoni iliyotoka sare ya 2-2 na Clove kusonga mbele Robo Fainali moja kwa moja kutoka Kundi A.
    Uchawi wa Mbeya hauvuki bahari; Mbeya City timu tishio Bara imegeuzwa nyanya visiwani

    Katika mechi ya awali ya Kundi C, Uwanja wa Amaan, Tusker ya Kenya ilikata tiketi ya Robo Fainali pia baada ya kuifunga Spice Stars mabao 2-0, hivyo inaungana na Azam FC kufuzu moja kwa moja Robo Fainali kutoka kundi hilo.
    Clove yenye pointi mbili, inaungana na KMKM na Ashanti United zenye pointi moja moja kuwania nafasi mbili za timu zilizomaliza na wastani mzuri katika nafasi ya tatu kutoka makundi yote, ili kuingia Robo Fainali.
    Mechi ya mwisho ya makundi inachezwa usiku wa leo Uwanja wa Amaan, kati ya mabingwa watetezi Azam FC dhidi ya Ashanti United.
    Mbeya iliyopanda Ligi Kuu ya Bara msimu huu na kuwa moja ya timu zilizo kwenye mbio za ubingwa, haikuwahi kufungwa hata mechi moja kabla ya Kombe la Mapinduzi. Inaondoka Pemba baada ya kutoa sare moja na Clove 1-1 na kufungwa mechi mbili na Chuoni 2-1 na URA 1-0.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: 'UCHAWI' WA MBEYA CITY HAUVUKI BAHARI, YATOLEWA MAPEMA KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top