• HABARI MPYA

    Saturday, January 18, 2014

    COASTAL UNION YATOA SARE NA SEEB

    Na Mahmoud Zubeiry, Muscat
    COASTAL Union imelazimishwa sare ya bila kufungana na Seeb Club ya Oman kwenye Uwanja wa Seeb, mjini Muscat jioni hii katika mchezo mzuri wa kirafiki.
    Ikimtumia mshambuliaji aliye majaribioni kutoka Ruvu Shooting ya Tanzania, Elias Maguri, Seeb ilionyesha upinzani mkali kwa Coastal tangu mwanzo hadi mwisho wa mchezo.
    Seeb walikuwa wakicheza kwa kupiga pasi nyingi za haraka uwanjani, wakati Coastal ilitumia mipira mirefu na mashambulizi ya kutokea pembeni.
    Mshambuliaji wa Coastal Union, Atupele Green akiwania mpira dhidi ya mabeki wa Seeb leo

    Haruna Moshi ‘Boban’ aliyeanza pamoja na Mganda Yayo Lutimba mbele waliisumbua ngome ya Seeb na Danny Lyanga na Atuepele Green waliwasumbua mabeki wa pembeni wa timu hiyo ya katikati ya jiji a Muscat.
    Baada ya mchezo wa leo, Coastal itacheza mechi moja zaidi na timu ambayo itatajwa baadaye, kufuatia Al Thuwaiq kugoma kucheza nao kwa madai hawakuwa na taarifa za uhakika.
    Katika mechi zake tatu za awali, Coastal ilizifunga 2-0 kila timu Nadi Oman na Musannaa kabla ya kufungwa 1-0 na Fanja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL UNION YATOA SARE NA SEEB Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top