• HABARI MPYA

    Saturday, January 18, 2014

    MTIBWA SUGAR YAWAKALISHA SIMBA SC TAIFA, LOGARUSIC NYWIIIIIIII

    Na Princess Asia, Dar es Salaam
    BAO pekee la Masoud Ally ‘Chile’, jioni hii limeipa ushindi wa 1-0 Mtibwa Sugar ya Morogoro dhidi ya Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki.
    Masoud alifunga bao hilo akimalizia pasi nzuri ya kiungo wa pembeni Jamal Mnyate dakika ya 64 ya mchezo huo mkali na wa kusisimua. 
    Huo ni mchezo wa pili mfululizo Simba SC kufungwa chini ya kocha mpya, Mcroatia, Zdravko Logarusic baada ya awali kufungwa na KCC ya Uganda katika ya Kombe kla Mapinduzi.

    Awali, Logarusic aliiongoza Simba SC kushinda mechi saba mfululizo, ikiwemo ya Nani Mtani Jembe dhidi ya wapinzani, Yanga SC mabao 3-1.
    Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Yaw Berko, William Lucian ‘Gallas’/Nassor Masoud ‘Chollo’, Omar Salum/Adeyoum Saleh, Gilbert Kaze, Donald Mosoti, Awadh Juma, Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Edward Christopher, Betra Mombeki/Zahor Pazi, Ali Badru na Said Ndemla.
    Mtibwa Sugar; Hussein Sharrif ‘Casillas’, Said Mkopi ‘Mpiluka’, Paul Ngalema, Salvatory Ntebe, Salum Mbonde, Shaaban Nditi, Ally Shomary, Masoud Ally ‘Chile’, Juma Luizio, Jamal Mnyate, Ally Mohammed ‘Gaucho’/Vincent Barnabas.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAWAKALISHA SIMBA SC TAIFA, LOGARUSIC NYWIIIIIIII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top