TUNAZUNGUMZA sana kwenye vikao vyetu kuhusu wachezaji ambao tunaona kabisa wanaathirika kwa utumiaji wa dawa za kulevya. Hata baadhi ya mashabiki wamekwishagundua wachezaji fulani fulani, viwango vyao vinaathirika kwa utumiaji wa dawa za kulevya.
Taratibu idadi ya watumiaji mihadarati katika soka yetu inaongezeka na sasa vizazi na vizazi vinarithi desturi hii.
Miaka minne iliyopita, baada ya kushuka kwa kasi kwa kiwango cha soka Afrika Kusini kulilishitua mno Shirikisho la Soka nchini humo na hatua mbalimbali zikachukuliwa kuhakikisha mambo yanakaa vizuri tena.
Vipimo vinatembea na akibainika mchezaji anavuta bangi, amejifuta kwenye familia ya soka nchini humo. Ni hatua ya kupongeza kweli, sasa soka ya Afrika Kusini ipo kwenye kikombe cha matumaini mapya.
Vipi kwetu Tanzania? Tunafahamu fika kuna wachezaji wetu wamepigika kisoka kwa sababu ya utumiaji wa dawa za kulevya. Walianza kuvuta bangi, wakawa wavutaji kupindukia na sasa wanajidunga sindano za dawa za kulevya. Wamechoka.
Tena wale wale ambao miaka mitatu iliyopita tulikuwa tunawatabiria kucheza Ulaya, lakini sasa hali imebadilika na tunachowatabiria kwa sasa ni kutemwa wakati wowote kwenye klabu zao kadiri michango yao inavyozidi kupungua.
Wavuta bangi kwenye soka yetu, hao ni wengi sana na wengine wapo timu ya taifa pale. Tunawekeza nini kwenye soka yetu? Umefika wakati sasa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likachukua hatua za kupambana na hali hii.
Hii inapaswa kuingizwa kwenye kanuni na utaratibu wa kuwapima wachezaji wetu ukaanza mara moja. Tuweke kando ushabiki na tuwahukumu wachezaji bila kuwaangalia huyu ni wa klabu gani.
Kwani bila hivyo, na hawa wanaoibuliwa kwenye Copa Coca Cola nao watatumbukia tu kwenye janga hilo, iwapo hakutakuwa na tishio la kuwaogopesha kujitumbukiza kwenye utumiaji wa dawa za kulevya.
TFF iweke kanuni za adhabu, tena kali dhidi ya wachezaji watumiao dawa za kulevya nchini. Hii itakuwa njia nzuri ya kuwaengua wachezaji sumu kwenye soka yetu na kuondoa uwezekano wa kuambukiza wengine tabia hii.
Tunahitaji kujifunga mkanda na kupambana haswa kuhakikisha soka yetu inaimarika kwa kupigana katika kila nyanja, ili mambo yawe sawa. Tuanze kwa hili la dawa za kulevya, hususan bangi. Sidhani kama ipo timu ya Ligi Kuu ambayo inakosa wachezaji wasiopungua watatu wanaovuta bangi. Sidhani. Kwa kweli bangi zinaharibu sana wachezaji wetu na wengi wao bongo zao zimeoza bado wadogo tu.
Jambo zuri TFF ilipata uongozi mpya chini ya rais, Jamal Emil Malinzi mwishoni mwa mwaka jana aliyerithi kiti cha Leodegar Chilla Tenga, tunataka kuona, je naye ataachia bangi ziendelee kuua vipaji vya wanasoka wetu, au atachukua hatua kudhibiti hali hiyo?

.png)
0 comments:
Post a Comment