Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi, leo inaingia katika hatua ya Robo Fainali ka mechi nne kuchezwa kwenye viwanja viwili, Gombani, Pemba na Amaan, Zanzibar.
RATIBA ROBO FAINALI MAPINDUZI
KMKM Vs URA Saa 8:00 mchana (Gombani, Pemba)
Azam FC Vs Cloves Stars Saa 10:00 jioni (Gombani, Pemba)
KCC Vs Tusker Saa 10:00 jioni (Amaan, Zanzibar)
Simba SC Vs Chuoni Saa 2:00 Usiku (Amaan, Zanzibar).
WANAOONGOZA KWA MABAO MAPINDUZI
Owen Kasuule URA 3
Feni Ali URA 3
Amri Kiemba Simba 2
Brian Umony Azam 2
Mwinyi Mngwali Chuoni 2
Herman Waswa KCC 2
Kwenye Uwanja Gombani, mabingwa watetezi Azam FC watamenyana na Cloves Stars Saa 10:00 jioni, mechi itakayotanguliwa na mchezo mwingine wa hatua hiyo kati ya KMKM na URA ya Uganda.
Uwanja wa Amaan, Zanzibar mabingwa wa zamani wa michuano hiyo, Simba SC watamenyana na Chuoni ya Pemba kuanzia Saa 2:00 usiku, mechi itakayotangulia na mchezo mwingine kati ya KCC ya Uganda na Tusker ya Kenya.
Mgeni rasmi katika mchezo wa leo usiku Uwanja wa Amaan, anatarajiwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, ambaye ataongozana na Mjumbe wa Kamati yake ya Utendaji, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’.
Washindi wa mechi za leo watamenyana keshokutwa kusaka timu za kuingia Fainali Uwanja wa Amaan.
Fainali ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu itachezwa Januari 13 Uwanja wa Amaan.




.png)
0 comments:
Post a Comment