• HABARI MPYA

    Friday, January 17, 2014

    TFF YANOA MAKATIBU MABORESHO TAIFA STARS

    Na Boniface Wambura, Ilala
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeandaa semina ya siku mbili kwa makatibu wa vyama vya soka vya mikoa kuhusu maboresho ya timu ya Taifa (Taifa Stars).
    Semina hiyo inafanyika ukumbi wa Singida Motel, mjini Singida kuanzia kesho (Januari 18 mwaka huu) ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa kwa washiriki kuhusu maboresho hayo.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameapania kuinua soka ya Tanzania

    TFF imeandaa mpango wa maboresho kwa Taifa Stars ambapo pamoja na mambo mengine umepanga kusaka vipaji nchini nzima kwa lengo la kupanua wigo wa kupata wachezaji wanaoweza kuchezea timu hiyo.
    Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager mwaka huu inakabiliwa na mechi za mchujo za Kombe la Afrika (AFCON) ambalo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Morocco.
    Mechi hizo za mchujo zitachezwa kati ya Septemba na Novemba mwaka huu ili kupata timu 16 zitakazofuzu kucheza fainali hizo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YANOA MAKATIBU MABORESHO TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top