• HABARI MPYA

    Saturday, November 01, 2014

    CHELSEA RAHA PALE PALE, QPR AFA 2-1...THE BLUES 'YALA BATA' KILELENI

    CHELSEA imejiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Queens Park Rangers jioni ya leo Uwanja wa Smtamfrod Bridge, London.
    Ushindi huo, unaifanya timu ya Jose Mourinho itimize pointi 26 baada ya kucheza mechi 10,ikiizidi kwa pointi nne Southampton katika nafasi ya pili na pointi tisa mabingwa watetezi, Manchester City walio nafasi ya tatu.
    Oscar dos Santos Emboaba Junior aliifungia bao la kwanza The Blues dakika ya 32 kabla ya Charlie Austin kuisawazishia QPR dakika ya 62- na Eden Hazard kufunga la ushindi kwa penalti dakika ya 75.
    Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Filipe Luis, Matic, Fabregas, Willian/Drogba dk64, Oscar, Hazard/Ramires dk90 na Diego Costa/Schurrle dk78.
    QPR; Green, Isla, Caulker, Dunne, Suk-Young, Vargas, Henry, Sandro, Fer/Traore dk83, Hoilett/Zamora dk60 na Austin.

    Eden Hazard akishangilia baada ya kuifungia Chelsea bao la ushindi dhidi ya QPR

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2816991/Chelsea-2-1-QPR-Eden-Hazard-slots-home-second-half-penalty-edge-struggling-Rangers-west-London-derby.html#ixzz3Hq114lJ7 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA RAHA PALE PALE, QPR AFA 2-1...THE BLUES 'YALA BATA' KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top