• HABARI MPYA

    Tuesday, May 05, 2015

    ETOILE YAPEWA TIMU ILIYOIFUNGA YANGA 6-0 KOMBE LA SHIRIKSHO

    WABABE wa Yanga SC, Etoile du Sahel ya Tunisia wamepangwa kucheza na Raja Athletic Club ya Morocco katika mechi ya mchujo kuwania kupangwa Kombe la Shirikisho Afrika.
    Yanga SC ilitolewa na Etoile katika hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho baada ya kufungwa bao 1-0, ikitoka kulazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam.
    Raja imewahi kupangwa na Yanga SC katika Kundi B la Ligi ya Mabingwa 1998 na mechi ya kwanza ilishinda 6-0 mjini Cassablanca, wakati marudiano Watoto wa Jangwani walilazimishwa sare ya 3-3 Dar es Salaam.

    Katika upangaji wa droo za mashindano yote ya CAF leo mjini Cairo, Misri iliyoongozwa na Katiku MKuu wa shirikkisho hilo, Hicham El Amrani aliyesaidiwa na Makamu wa kwanza wa Rais, Suketu Patel, Makamu wa Pili, Almamy Kabele El Ahly ya Misiri itacheza na Club Africain ya Tunisia, 
    Esperance ya Tunisia na Hearts of Oak ya Ghana, 
    AC Leopards ya Kongo na Warri Wolves ya Nigeria, 
    CS Sfaxien ya Tunisia na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
    AS Vita ya DRC itamenyana na Stade Malien ya Mali, Orlando Pirates ya Afrika Kusini na AS Kaloum ya Guinea, Zamalek ya Misri na Sanga Balende  ya DRC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ETOILE YAPEWA TIMU ILIYOIFUNGA YANGA 6-0 KOMBE LA SHIRIKSHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top