• HABARI MPYA

    Tuesday, May 05, 2015

    TP MAZEMBE YAPEWA VIBONDE KUNDI A, TIMU TATU ZA ALGERIA ZAPANGWA PAMOJA KUNDI B

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    TP Mazembe imepangwa na timu inazozimudu katika Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika, Al HIlal ya Sudan na timu nyingine mbili zinazocheza kwa mara ya kwanza michuano hiyo, Moghreb Tetouane ya Morocco na Smouha ya Misri.
    Katika droo ya michuano hiyo iliyopangwa leo mjini Cairo, Misri, historia imetengenezwa kwa timu tatu za Algeria kupangwa pamoja kundi moja, B.
    Mabingwa watetezi, ES Setif na Waalgeria wengine USM Alger na MC Eulma wameangukia kundi B na El Merreikh ya Sudan.

    Hii ni mara ya kwanza klabu tatu za nchi mmoja kutinga ligi ndogo ya Mabingwa Afrika na historia inanoga zaidi baada ya timu hizo kupangwa kundi moja.
    Hivi karibuni imeshuhudiwa timu mbili kama TP Mazembe na AS Vita za DRC zikipangwa kundi moja katika Ligi ya Mabingwa kama ilivyokuwa kwa wapinzani wa hadi wa Misri, Ahly na Zamalek. 
    Mabingwa mara nne wa Afrika, TP Mazembe wamepangwa Kundi A pamoja na El Hilal ya Sudan, Moghreb Tetouane ya Morocco na Smouha ya Misri.
    Mazembe yenye washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu inaweza kupata tabu kidogo kwa Hilal, lakini si wapinzani wengine katika kundi lake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TP MAZEMBE YAPEWA VIBONDE KUNDI A, TIMU TATU ZA ALGERIA ZAPANGWA PAMOJA KUNDI B Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top