BONDIA Floyd Mayweather amesema kwamba atakuwa tayari kwa pambano la marudiano Manny Pacquiao mwakani.
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 38 alishinda kiulaini kwa pointi dhidi ya Pacquiao Alfajiri ya Jumapili ukumbi mjini Las Vegas, Marekani.
Lakini baada ya pambano hilo lililofanyika ukumbi wa MGM Grand, imegundulika kwamba Mfilipino alikuwa ana maumivu ya bega ambayo sasa yanataka upasuaji.
Mayweather akiwa na mikanda yake baada ya kumshinda Pacquiao ukumbi wa MGM Grand Garden Arena
Na Mayweather, ambaye sasa amefikisha mapambano 48 na ameshinda yote, ameiambia ESPN kwamba atakuwa tayari kwa pambano la marudiano na Pacquiao akimaliza upasuaji wake.
"Nitapigana naye mwakani baada ya upasuaji wake,' amesema Mayweather akimuambia mwandishi wa ESPN, Stephen A. Smith kwa ujumbe wa maandishi kwa simu.
Awali, bondia huyo mbabe wa uzito wa Welter asiyepingika alisema atapigana pambano moja zaidi mwezi Septemba kabla ya kustaafu
Floyd Mayweather amesema yuko tayari kwa pambano la marudiano na Manny Pacquiao mwakani
0 comments:
Post a Comment