Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KIUNGO mshambuliaji, Mrisho Khalfan Ngassa leo atacheza kwa mara ya mwisho akiwa na jezi ya Yanga SC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati timu hiyo itakapokuwa ikimenyana na timu yake ya zamani, Azam FC.
Yanga SC wanamenyana na Azam FC katika mchezo wa kukamilisha ratiba, baada ya kuwa tayari imekwishajihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mchezo huo ni muhimu kwa Azam kushinda ili kujihakikishia nafasi ya pili, lakini Yanga SC hawatapenda kukabidhiwa Kombe la ubingwa wakitoka kufungwa na mabingwa hao wa zamani.
Na Mrisho Ngassa ambaye amemaliza Mkataba wake Yanga SC anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo kwenda kutafuta changamoto mpya, ingawa bado haijajulikana atakwenda timu gani, japo magazeti yamekuwa yakiandika anahamia Afrika Kusini.
Ngassa ataondoka Yanga SC baada ya kuichezea jumla ya mechi 185 katika awamu mbili, na kuifungia jumla ya mabao 86.
Ngassa aliyetimiza miaka 26, Aprili 12 mwaka huu, alijiunga na Yanga SC mwaka 2006, akitokea Kagera Sugar iliyomuibua mwaka 2005 kutoka timu ya vijana ya Toto Africans ya Mwanza.
Mwaka 2010 alihamia Azam FC kwa dau la rekodi wakati huo, dola za Kimarekani 40,000 (Sh. Milioni 80).
Kabla ya hapo, akiwa Yanga SC, Aprili mwaka 2009, Ngassa alikwenda kufanya majaribio klabu ya Ligi Kuu England, West Ham United wakati huo chini ya kocha Mtaliano Gianfranco Zola.
Hata hivyo, pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Zola kuvutiwa na uwezo wa mchezaji huyo kisoka, akasema Ngassa anahitaji kurejea Afrika kuongeza lishe.
Julai mwaka 2011, Ngassa alikwenda kufanya majaribio Seattle Sounders FC ya Ligi Kuu ya Marekani na akatumiwa katika mchezo wa kujiandaa na msimu dhidi ya Manchester United ya England.
Hata hivyo, Azam FC haikuwa tayari kumuuza mchezaji huyo. Ngassa alicheza Azam FC hadi mwaka 2012 alipohamia Simba SC kwa mkopo na mwaka 2013 akarejea timu yake kipenzi, Yanga SC ambako leo atawapungia mkono mashabiki baada ya mechi kuwaamnia ‘kwaherini’.
KIUNGO mshambuliaji, Mrisho Khalfan Ngassa leo atacheza kwa mara ya mwisho akiwa na jezi ya Yanga SC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati timu hiyo itakapokuwa ikimenyana na timu yake ya zamani, Azam FC.
Yanga SC wanamenyana na Azam FC katika mchezo wa kukamilisha ratiba, baada ya kuwa tayari imekwishajihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mchezo huo ni muhimu kwa Azam kushinda ili kujihakikishia nafasi ya pili, lakini Yanga SC hawatapenda kukabidhiwa Kombe la ubingwa wakitoka kufungwa na mabingwa hao wa zamani.
Na Mrisho Ngassa ambaye amemaliza Mkataba wake Yanga SC anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo kwenda kutafuta changamoto mpya, ingawa bado haijajulikana atakwenda timu gani, japo magazeti yamekuwa yakiandika anahamia Afrika Kusini.
![]() |
Mrisho Ngassa anatarajiwa kuwapa mkono wa kwaheri mashabiki wa Yanga SC leo |
Ngassa ataondoka Yanga SC baada ya kuichezea jumla ya mechi 185 katika awamu mbili, na kuifungia jumla ya mabao 86.
Ngassa aliyetimiza miaka 26, Aprili 12 mwaka huu, alijiunga na Yanga SC mwaka 2006, akitokea Kagera Sugar iliyomuibua mwaka 2005 kutoka timu ya vijana ya Toto Africans ya Mwanza.
Mwaka 2010 alihamia Azam FC kwa dau la rekodi wakati huo, dola za Kimarekani 40,000 (Sh. Milioni 80).
Kabla ya hapo, akiwa Yanga SC, Aprili mwaka 2009, Ngassa alikwenda kufanya majaribio klabu ya Ligi Kuu England, West Ham United wakati huo chini ya kocha Mtaliano Gianfranco Zola.
Hata hivyo, pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Zola kuvutiwa na uwezo wa mchezaji huyo kisoka, akasema Ngassa anahitaji kurejea Afrika kuongeza lishe.
Julai mwaka 2011, Ngassa alikwenda kufanya majaribio Seattle Sounders FC ya Ligi Kuu ya Marekani na akatumiwa katika mchezo wa kujiandaa na msimu dhidi ya Manchester United ya England.
![]() |
Ngassa kushoto anatarajiwa kuhamia Afrika Kusini kwa mujibu wa taarifa za magazeti |
0 comments:
Post a Comment