KUNA stori ilikuwa inaendelea Yanga SC siku za karibuni, kwamba wachezaji wao wapya, Kpah Sherman kutoka Liberia na Mrundi Amissi Tambwe walilogwa na wachezaji wenzao ili wasiwe wanafunga mabao.
Eti kuanza kwao kufunga katika Ligi Kuu kulitokana na wachezaji hao kupelekwa kwa wataalamu wakafunguliwa miguu waweze kufunga.
Tambwe aliingia Yanga SC akiwa ametoka kuwa mfungaji bora katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na klabu ya Simba, ambayo ilimtema Desemba.
Sherman aliiingia Yanga SC na rekodi nzuri ya mabao kuanzia Liberia hadi Cyprus Kaskazini alipokuwa anacheza kabla ya kuja Tanzania.
Wote wakajikuta na mwanzo mgumu Jangwani, kutokana na kukosa mabao ya wazi katika mechi za Kombe la Mapinduzi na baadaye Ligi Kuu.
Lakini baada ya muda Tambwe akaanza kufunga na Sherman akafuatia. Stori ikawa wamefunguliwa miguu.
Miaka mitatu iliyopita, iliwahi kuripotiwa mshambuliaji Mrundi, Didier Kavumbangu aligombana mazoezini na mchezaji mwenzake, Jerry Tegete akimtuhumu anamloga.
Hali hiyo ilitokana na Kavumbangu aliyeingia na rekodi nzuri ya mabao Yanga SC kutoka Atletico ya kwao Burundi, kupoteza shabaha.
Lakini msimu uliofuata Kavumbangu akaanza kufunga na kuwa mmoja wa wafungaji tegemeo wa timu hadi anaondoka kwenda Azam FC msimu huu.
Simon Msuva hakuwa anafunga sana katika misimu yake miwili yake miwili ya mwanzo, lakini hadi sasa ndiye anaongoza kwa mabao Ligi Kuu, 17 akifuatiwa na Tambwe 14.
Wakati Yanga SC inafungwa 1-0 na Etoile du Sahel mjini Sousse katika mchezo wa marudiano, wote Tambwe na Sherman walipata nafasi nzuri za kufunga wakakosa mabao.
Katika eneo lile lile ndani ya boksi, Tambwe alipatwa na kigugumizi cha mguu baada ya krosi Mrisho Ngassa hadi akapokonywa mpira, wakati Tambwe akimpasia kipa mikononi.
Bado stori ni eti wachezaji hao ‘hawajafunguliwa vizuri’- ndiyo maana wanakosa mabao.
Mbaya zaidi stori hizi zinaletwa na wanachama wenyewe wa Yanga SC, tena wale walio karibu na timu.
Mambo mawili makubwa na mabaya wanayafanya hapa, kwanza wanawachonganisha wachezaji kwa wachezaji na kuondoa umoja katika timu.
Lakini pili, wanawakatisha tamaa wachezaji, kwani badala ya kufikiria kitu bahati mbaya, au hali ya kimchezo baada ya kukosa mabao, wataanza kuona Yanga ni timu ngumu kuchezea.
Hili ni jambo la kukemewa na wanaopaswa kufanya hivyo ni viongozi wa Yanga SC, wawakanye wanachama wenye tabia hizo.
Wachezaji wote duniani wakati fulani hupitia kipindi kigumu, na wanaoshindwa kumudu presha ya hali hakisi hushindwa kabisa kurejea katika viwango vyao.
Radamel Falcao alisajiliwa kwa mkopo Manchester United Septemba mwaka jana akiwa na rekodi nzuri ya mabao kuanzia River Plate aliyojiunga nayo mwaka 2011 akitokea Lanceros Boyaca ambayo aliifungia mabao 34 katika mechi 90.
FC Porto aliyojiunga nayo mwaka 2009, aliifungia mabao 41 katika mechi 51, kabla ya mwaka 2011 kuhamia Atletico Madrid alikofunga mabao 52 katika mechi 68- hivyo kununuliwa kwa dau la Euro Milioni 60 Monaco mwaka 2013, ambaako pamoja na kuandamwa na majeruhi, lakini aliweza kufunga mabao 11 katika mechi 20.
Hata hivyo, makali ya Falcao yamezidi kufifia baada ya kutua kwa mkopo, kwani mechi 24 amefunga manne tu hadi sasa.
Robin van Persie aliingia Manchester United na rekodi nzuri ya mabao mwaka 2012 ambayo akafanikiwa kuiendeleza katika misimu miwili ya mwanzoni.
Lakini msimu huu, van Persie amepoteza shabaha. Alikuwa ndiye mchezaji anayeaminiwa zaidi kupiga penalti tangu Arsenal.
Lakini mwishoni mwa wiki akakaosa penalti, Manchester United ikifungwa 1-0 na West Bromwich Albion katika Ligi Kuu Englamd na kocha Louis van Gaal akamnyang’anya jukumu la kupiga matuta.
Ukweli ni kwamba kuna wakati wachezaji wanapitia vipindi vigumu na inapotokea hali hiyo wanahitaji zaidi kujengwa kusaikolojia kuliko kuchanganywa na habari za kuzishi na kizandiki eti wanalogwa.
Jerry Tegete yupo katika wakati mgumu hivi sasa Yanga SC, hafungi mabao na hapangwi katika mechi kutokana na kila anapopewa nafasi, hafungi. Huyo nani anayemloga?
Huko nisizame ndani, tujiulize nani anayemloga Van Persie kwa sasa hafungi. Nani anayemloga Falcao?
Wakati umefika klabu zisaidie kuwabadilisha wachezaji wetu kwanza kuanza zenyewe kuacha ushirikina. Nilishasema hausaidii na kama unasaidia kwa nini timu ikifungwa hawafukuzwi waganga bali makocha na timu inatafuta wachezaji wengine bora zaidi wa kusajili.
Mpira wa miguu ni sayansi- ambayo haina miujiza inayoifikiriwa, eti ya ushirikina.
Kama klabu inawashirikisha wachezaji katika imani za kishirikina ili timu ishinde, tarajia hata mchezaji naye atafanya ushirikina kujiweka. Na hapo huwezi kukosa ugomvi kama huu wa mchezaji analogwa na mchezaji mwenzake.
Haya mambo ni huku kwetu tu Afrika, lakini kwa wenzetu waliopiga hatua kubwa mbele, hakuna. Nani anawaloga Falcao na Van Persie pale United?

0 comments:
Post a Comment