• HABARI MPYA

    Wednesday, May 06, 2015

    SIMON MSUVA ‘AKWEA PIPA’ KWENDA KUJARIBU BAHATI ORLANDO PIRATES

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    WINGA wa Yanga SC, Simon Msuva ameondoka leo kwenda Afrika Kusni kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya Orlando Pirates ya huko.
    Msuva aliomba ruhusa kwa uongozi wa Yanga jana wakamkatalia, lakini leo amepanda ndege kwenda Johannesburg.
    Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba Pirates walileta mwaliko wa majaribio kwa ajili ya Msuva, lakini wakamuambia asubiri amalize Ligi Kuu atakwenda.
    “Najua kuna hiyo safari, ila aliambiwa asuburi amalize Ligi atakwenda, kama amekwenda bila ruhusa atakuwa amefanya makosa,”amesema Muro. 
    Simon Msuva ameondoka leo kwenda Afrika Kusini

    Msuva aliyeibukia akademi ya Azam FC, ameondoka akiwa tayari ameipa Yanga SC ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, huku pia akiwa anaongoza kwa mabao, 17 akifuatiwa na mchezaji mwenzake wa timu hiyo, Amissi Tambwe mabao 14.   
    Tangu ajiunge na Yanga SC mwaka 2012 akitokea Moro United, Msuva ameifungia timu hiyo mabao 35 jumla katika mechi 102 za mashindano yote.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMON MSUVA ‘AKWEA PIPA’ KWENDA KUJARIBU BAHATI ORLANDO PIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top