• HABARI MPYA

    Monday, June 11, 2012

    STEWART AWASILI LEO KUANZA KUISUKA AZAM YA UBINGWA KAGAME


    KOCHA Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall anatarajiwa kuwasili nchini leo asubuhi kwa ajili ya kuanza program ya maandalizi kwa mashindano ya kombe la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
    Stewart alikuwa nchini Uingereza kwa mapumziko baada ya kumaliza msimu uliopita kwa mafanikio ya kutwaamedali ya fedha kwa kuwa  washindi wa pili wa VPL.
    Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrissa jana ameiambia tovuti ya http://www.azamfc.co.tz/  kuwa  wataanzamazoezi jioni kutokana na kocha huyo kurudi asubuhi ya siku hiyo.
    Akizungumzia wachezaji wengine alisemawachezaji wote wa kimataifa wameshawasili tayari kwa kuanzamazoezi hayo wakiwa pamoja na wachezaji wengineMazoezi hayo yatafanyika  kwenye uwanja wa AzamChamazi jijini Dar es Salaam.
    Idrissa aliongeza kuwa wachezaji waliopo timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ watajiunga mara baada yakumaliza michezo yaona wale wa Zanzibar Heroes watarejea nchini baada ya kumaliza michezo ya Kombe laDunia kwa nchini ambazo sio wanachama wa FIFA.
    Aliwataja wachezaji waliowasili kuwa ni George Odhiambo na Ibrahim Shikanda kutoka nchini Kenya ambao wotewaliingia AlhamisTchetche Kipre na Michael Kipre kutoka nchini Ivory na Joseph Owino wa Uganda.
    Idrissa alisema wachezaji wa Tanzania nao wameshaandaa mazingira kwa ajili ya kuanza mazoezi hayowakiwemo vijana kutoka Azam Academy ambao wamepanda kuicheza timu kubwaAishi SalumJucksonWandwiDizana Issa, Ibrahim Rajab ‘Jeba’ na Joseph Kimwaga.
    Aidha Idrissa alisema Azam Academy wameshaanza mazoezi siku ya Ijumaa isipokuwa wacheza watatu ambaobado hawajawasili kujiunga na timu hiyo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STEWART AWASILI LEO KUANZA KUISUKA AZAM YA UBINGWA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top