• HABARI MPYA

    Tuesday, October 16, 2012

    MBAGA AZICHEZESHA KENYA, BAFANA BAFANA

    Oden Mbaga kulia akimuonya Haruna Moshi 'Boban' wakati wa mechi kati ya Taifa Stars na Malawi, Mei 26, mwaka huu. Kulia ni kiungo wa The Flames, James Sangala aliyechezewa rafu na Haruna.

    Na Prince Akbar
    REFA Oden Mbaga wa Tanzania anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ndiye anayechezesha mechi ya kirafiki kati ya Kenya (Harambee Stars) na Afrika Kusini (Bafana Bafana).
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba mechi hiyo inachezwa leo Uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani jijini Nairobi na Mbaga atasaidiwa na marefa wasaidizi wa FIFA, John Kanyenye kutoka Mbeya na Erasmo Jesse wa Morogoro.
    Amesema TFF imeteua marefa hao baada ya kupata maombi kutoka kwa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) ambao ndiyo waandaaji wa mechi hiyo ambayo ni moja ya vipimo kwa kocha mpya wa Harambee Stars, Henry Michel kutoka Ufaransa.
    Wakati huo huo: Wambura Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Makocha wa Soka Tanzania (TAFCA) imeongeza muda kwa wagombea kuchukua fomu kwa ajili ya uchaguzi wa chama hicho ambao sasa utafanyika Novemba 25 mwaka huu.
    Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA, Ramadhan Mambosasa, jana ndiyo ilikuwa mwisho wa kuchukua fomu lakini mwitikio wa wagombea bado umekuwa mdogo ambapo ni watano tu waliojitokeza.
    Hivyo, amesema wameongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu ambapo mwisho itakuwa ni Oktoba 19 mwaka huu saa 10 kamili alasiri. Fomu zinapatikana ofisi za TAFCA ambazo ziko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
    Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, Mhazini na wajumbe watatu wa Kamati ya Utendaji.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MBAGA AZICHEZESHA KENYA, BAFANA BAFANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top