Marehemu Ally Suleiman 'Aurora' |
PROMOTA wa ngumi nchini, Ally Suleiman 'Aurora' aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana, amezikwa leo kwenye makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.
Taarifa ya ndugu za marehemu, aliyekuwa mmiliki wa kampuni ya Aurora Security, imesema Ally alifikwa na mauti baada ya kuugua kwa muda mrefu na kulazwa kwenye hospital ya Muhimbili.
Pamoja na kuwa promota wa ngumi, enzi za uhai wake Aurora pia aliweza kufadhili mashindano ya urembo, sambamba na michezo mbalimbali, ikiwemo timu ya Waandishi wa Habari za Michezo na Burudani nchini, TASWA FC.
Miongoni mwa mabondia waliofanikiwa kwa msaada wa Aurora ni bingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Awadh Tamim ambaye alisaidiwa na Aurora kutimiza ndoto hizo.
0 comments:
Post a Comment