![]() |
Jenerali Banza Stone |
MWANAMUZIKI nyota wa dansi nchini, Ramadhani Masanja ‘Banza
Stone’ ameomba kurudi bendi yake ya zamani, African Stars ‘Twanga Pepeta’ ili
aokoe jahazi, akisema ana machungu na bendi hiyo na hapendi kuona inayumba.
Banza alipandaa jukwaa la Twanga Pepeta usiku wa jana kwenye
ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, huku bendi yake, Extra Bongo ikitumbuiza
kwenye ukumbi wa Meeda, Sinza, Dar es Salaam.
Banza alikuwapo tangu mwanzo wa onyesho la Twanga hadi
mwisho na alipopanda jukwaani kuimba, ukumbi mzima uliripuka kwa mayowe ya kumshangilia
na alituzwa fedha nyingi wakati akipiga rap ya Pinda Mugongo.
Baada ya hapo, Banza alisogea faragha na Mkurugenzi wa
Twanga Pepeta, Asha Ramadhani Baraka na habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata
mchana huu kutoka ndani ya uongozi wa bendi hiyo, zimesema kwamba gwiji huyo na
mwasisi wa bendi ameomba rasmi kurudi nyumbani.
“Kimsingi Asha amekubali, kilichobaki ni kusaini mkataba tu,
ingawa Banza mwenyewe anataka kurudi hata bila mkataba, ila kwa ushindani wa
sasa wa kibiashara katika bendi ulivyo, lazima asainishwe mkataba,”alisema
kiongozi mmoja wa bendi hiyo.
Wanamuziki wa Twanga pia wamefurahia habari za kurejea Banza
wakiamini kwa utunzi wake bora, upangiliaji wa muziki na ubunifu wa hali ya juu
alionao, bendi hiyo itaendelea kuwa juu chini ya Jenerali mwana wa Masanja.
Banza ni mwasisi wa Twanga na alishiriki kikamilifu albamu
ya kwanza ya bendi hiyo, Kisa cha Mpemba
na wakati akiwa amekamilisha maandalizi ya albamu ya pilia, Jirani, akachukuliwa na TOT Plus na hapo
ndipo akampa nafasi Ally Choky kupata umaarufu katika bendi hiyo.
Banza aliwahi kurejea Twanga mwaka ilipoyumba, baada ya
Choky kuondoka, lakini baadaye Choky aliporejea yeye akapelekwa bendi ya pili,
Twanga Chipolopolo ambako hata hivyo nako hakudumu akaenda kuanzisha bendi
yake, Bambino Sound.
Kufa kwa Bambino kulimfanya Banza aungane tena Choky kufufua
bendi ya Extra Bongo na sasa inaonekana ameamua kuachana na Kamarade, Mtoto wa Lwambo
na kurejea nyumbani.
Kwa sasa tayari Extra Bongo imekwishaanza kuyumba na wanamuziki
wengi wanalalamikia hali ngumu- huku rapa Ferguson akiwa amekwishafungua milango
ya kukimbia ‘waya’ kwa kutimkia Mashujaa Band, inayokuja kwa kasi.
DADA YAKE TEDI MAPUNDA ALIVYOAGWA KABLA YA MAZISHI SHINYANGA
DADA YAKE TEDI MAPUNDA ALIVYOAGWA KABLA YA MAZISHI SHINYANGA
Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda akizungumza na Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti nyumbani kwake Mbezi Beach Teddy Mapunda amefiwa na mdogo wake marehemu Noela aliyerafiki juzi na kusafirishwa jana kwenda Shinyanga kwa mazishi, kulia ni Mkurugenzi wa Radio One na ITV B. Joyce Mhavile.
Mwili wa Marehemu Noela ukiingizwa nyumbani kwao kwa sala kabla ya kusafirishwa kuelekea mkoani Shinyanga kwa mazishi.
Mama Tunu Pinda akiongoza waombolezaji wakati wa maombo kwa ajili ya marehemu katika msiba huo.
Baadhi ya ndugu wa marehemu wakiwa katika ibada hiyo jana.
Bw. Nestor Mapunda kulia Shemeji wa marehemu Noela akiwa amekaa pamoja na Rais wa TFF Leodger Tenga katikati.
Padri akiongzoa waombolezaji katika swana ya kumuombea marehemu Noela.
Mama Tunu Pinda akimfariji Teddy Mapunda wakati alipokuwa akimlilia marehemu mdogo wake Noela wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu nyumbani kwake Mbezi Beach.
Waombolezaji ndugu na jamaa wakilia kwa uchungu wakati wa kuaga mwili wa marehemu.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Ephraim Mafuru katika akijumuika napamoja na waombolezaji wengine katika msiba huo.
Mama Pinda akitoa heshima zake za mwisho kwa marehemu Noela .
Teddy Mapunda akifarijiwa na Nandi Mwiyombela huku akilia kwa uchungu wakati akiaga mwili wa marehemu mdogo wake.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Ephraim Mafuruna Rais wa TFF Leodger Tenga wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Noela.
Mkurugenzi wa Fullshangwe John Bukuku akipita kutoa heshimza za mwisho kwa mwili wa marehemu Noela.
Teddy Mapunda akitoa heshima za mwisho kwa marehemu mdogo wake Noela.
Wazazi wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu Noela.
0 comments:
Post a Comment