Beki kinda la Liverpool laitwa kikosini kuziba pengo Euro 2012.
BEKI wa England, Gary Cahill ameondolewa kwenye kikosi cha Euro 2012 baada ya kupasuka mara mbili kwenye taya.
Beki huyo wa kati wa Chelsea aliumia katika mechi ya kirafiki na Ubelgiji, baada ya kugongana na kipa wake, Joe Hart Jumamosi.
Mchezaji wa Liverpool, Martin Kelly ameitwa kuziba nafasi hiyo.
Beki mwenzake, John Terry anayesumbuliwa maumivu ya nyama za paja, ameruhusiwa kurudi uwanjani baada ya kutibiwa.
Tayari kocha wa England, Roy Hodgson amekwishampoteza kipa John Ruddy (aliyevunjika kidole) sambamba na viungo Gareth Barry na Frank Lampard kwa majeruhi katika kikosi chake cha kwanza cha wachezaji 23.Taarifa ya FA imesema: "Cahill amevunjika taya mara mbili.
Beki wa pembeni wa Liverpool, Kelly alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa akitokea benchi dhidi ya Norway mwishoni mwa wiki iliyopita na kinda huyo wa miaka 22 ameitwa mbele ya mabeki wazoefu, Micah Richards na Rio Ferdinand.
Nahodha wa zamani wa England, Ferdinand ameichezea mechi 81 timu ya taifa, lakini amefungiwa vioo na kocha Hodgson.
Kikosi cha England sasa:
Makipa: Joe Hart (Manchester City), Robert Green (West Ham), Jack Butland (Birmingham City).
Mabeki: Leighton Baines (Everton), Martin Kelly (Liverpool), Ashley Cole (Chelsea), Glen Johnson (Liverpool), Phil Jones (Manchester United), Joleon Lescott (Manchester City), John Terry (Chelsea), Phil Jagielka (Everton).
Viungo: Stewart Downing (Liverpool), Steven Gerrard (Liverpool), Jordan Henderson (Liverpool), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Scott Parker (Tottenham), Theo Walcott (Arsenal), Ashley Young (Manchester United).
Washambuliaji: Andy Carroll (Liverpool), Jermain Defoe (Tottenham), Wayne Rooney (Manchester United), Danny Welbeck (Manchester United).
0 comments:
Post a Comment