• HABARI MPYA

    Monday, June 04, 2012

    MAVETERANI WA REAL MADRID WAIPIGA 3-2 MAN UNITED

    Edwin van der Sar


    TIMU ya Maveterani ya Manchester United imefungwa mabao 3-2 na their Real Madrid katika mechi iliyojulikana kama Corazon Classic kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu usiku wa jana.
    Mechi hiyo ya hisani, kwa ajili ya kuchangia mfuko wa Real wa akademi za Afrika, iliyohusishwa wachezaji waliowika katika klabu hizo siku za nyuma, ilianza kwa burudani kubwa, Fernando Morientes akiwafungia wenyeji bao la kuongoza dakika ya saba, kabla ya Lee Sharpe kuwasawazishia Mashetani Wekundu ndani ya dakika ya mbiki.
    Luis Figo aliifungia tena Real, kabla ya kipa Edwin van der Sar kuokoa mchomo mmoja mkali sana wa Zinedine Zidane. Kipa aliyetokea benchi, Raimond van der Gouw naye aliinusuru timu yake kufungwa, baada ya kuokoa mchomo mkali akiwa amebaki yeye na Emilio Butragueno kipindi cha pili.
    Mkwaju wa penalti uliopigwa na Teddy Sheringham uliokolewa na Pedro Contreras, ambaye ndiye pia alimchezea rafu mshambuliaji huyo. Dakika mbili baadaye, wenyeji walipata ushindi wa 3-1 kwa bao la Fernando Redondo, aliyemtungua  van der Gouw.
    Sheringham alikosa bao la wazi zikiwa zimebaki dakika 10 wakati mshambuliaji wa zamani wa England, Andy Cole naye alipoteza nafasi nzuri mno.
    Kiksi cha Man United: Van der Sar (Van der Gouw 62), Martin (Thomas 77), Johnsen, Dublin, Irwin; Blomqvist (Robson 77), Yorke, Fortune, Sharpe (Blackmore 61); Cole, Sheringham.


    SUGU, PROF JAY, NATURE WALIVYOPAGAWISHA DAR LIVE

    Gwiji wa Hip hop, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Mr II' a.k.a Sugu, juzi alizikonga nyoyo za mashabiki wake waliofurika ndani ya ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam kwa kufanya makamuzi ya hatari katika tamasha la Usiku wa Sugu. Sugu alisindikizwa na Juma Nature, Profesa Jay, Vinega, Mkoloni na wengineo wengi kwenye shoo hiyo iliyokuwa ya aina yake.
    Katika picha juu Sugu akiwarusha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia leo. (picha zote kutoka Full Shangwe)
    Sugu na Mkoloni wakizidi kuwadatisha mashabiki.
    Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari nae akitoa 'verse' kuupamba usiku wa Sugu ndani ya Dar Live.
    Profesa Jay akiwapa burudani mashabiki wa Dar Live.
    Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi likifanya makamuzi stejini.
    Suma G nae alikuwepo kuupamba usiku huo.
    Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan akiwasalimia mashabiki wa Dar Live.
    Nyomi iliyohudhuria Usiku wa Sugu.
    Baadhi ya mashabiki wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Sugu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAVETERANI WA REAL MADRID WAIPIGA 3-2 MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top