Football | World Cup 2014
UAMUZI wa Argentina kutumia washambuliaji wake wote wanne 'babu kubwa' umezaa matunda, baada ya jana kufanikiwa kupata ushindi wa 4-0 dhidi ya Ecuador hivyo kuongoza mbio za kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil kwa nchi za Amerika Kusini.
Sergio Aguero, Gonzalo Higuain, Lionel Messi na Angel Di Maria wote walifunga mabao katiuka mchezo ambao, Argentina walipata mabao matatu ndani ya dakika 11 za kipindi cha kwanza.
Messi, alionyesha soka safi mno pengine kuliko anayoonyesha Barcelona na alikuwa nyota ya mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Monumental, mjini Buenos Aires.
"Tunatakiwa kuwa timu ngumu, imara katika ulinzi na hiyo itamfanya Lionel afanye mavitu yake kwa uhuru," alisema Alejandro Sabella.
Argentina inaongoza kundi la Amerika Kusini kwa pointi zake 10, baada ya kucheza mechi tano, ikiizidi pointi moja tu Chile, ambayo iliifunga Bolivia 2-0 mjini La Paz, na mbili zaidi dhidi ya Uruguay na Venezuela waliotoka sare ya 1-1 mjini Montevideo.
Pamoja na hayo, Argentina inawezwa kupitwa mwishoni mwa wiki ijayo, wakati wakicheza mechi ya kirafiki na wapinzani wao wakubwa na wenyeji wa fainali zijazo za Kombe la Dunia, Brazil nchini Marekani.
| |
0 comments:
Post a Comment