Football | Uefa Euro 2012TM
URENO ilipoteza nafasi kibao, ikiwemo Cristiano Ronaldo (pichani juu kushoto) kukosa penalti, katika mchezo ambao walitandikwa mabao 3-1 nyumbani na Uturuki jana, kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2012.
Kipigo hicho kinamaanisha kwamba, Ureno itaingia kwenye Euro 2012 baada ya kucheza mechi tatu bila kushinda hata moja. Pia walitoka sare ya 0-0 na Macedonia wiki iliyopita na wakatoka sare na wenyeji washirika wa Euro, Poland mwezi Februari. Ureno wapo Kundi B pamoja na timu kali tupu, Ujerumani, Uholanzi na Denmark.
|
0 comments:
Post a Comment