Kaburu akizungumza na kiungo anaepandishwa kutoka timu B, Jamal |
Maestro akizungumza na kipa wa Oljoro, Waziri |
Kocha wa Simba B, Abdallah Kibadeni akiwa kocha wa mazoezi ya viungo wa SImba A, Mganda Amatre Richard jioni hii Uwanja wa Kinesi |
Marefa wa mechi hiyo, Osman Kazi aliyekuwa akipuliza kipyenga kulia wakiwa wamepumzika wakati wa mapumziko |
Jioni hii, Simba SC imeanza mazungumzo na Waziri kwenye Uwanja wa Kinesi, Urafiki, Dar es Salaam, baada ya mechi ya kirafiki kati ya Simba B na Faru Dume iliyoisha kwa sare ya 1-1.
Waziri alikuwa mchezaji mualikwa katika kikosi cha Faru Dume na alidaka kwa umahiri mkubwa kiasi cha kuwavutia viongozi wa Simba, walioongozwa na Makamu Mwenyekiti wa klabu, Geoffrey Nyange 'Kaburu' na Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Simba SC, Ibrahim Masoud 'Maestro'.
Waziri ambaye mwaka juzi alichezea Majimaji ya Songea katika Ligi Kuu na iliposhuka Daraja akasajiliwa Oljoro, alisema makaba wake na timu hiyo ya jeshi la Kujenga Taifa unamalizika Juni 30, mwaka huu hivyo yuko huru kufanya mazungumzo na klabu nyingine.
Waziri mwenyewe ameonyesha nia ya kusajiliwa na Simba na amesema atafurahi kwenda kukutana na kipa hodari, Juma Kaseja akajifunze mengi.
Baada ya Barthez kusaini Yanga, Simba imebaki na makipa wawili, mbali na Kaseja mwingine na Albert
Mweta aliyesajiliwa msimu uliopita kutoka Toto African ya Mwanza, ambaye msimu huu hajadaka hata mechi moja katika kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.
Aidha, Kaburu ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba watawapandisha wachezaji wao watatu wa timu B katika kikosi cha kwanza, ambao ni Jamal Mwambeleko, Omar Salum na William Lucian.
Wachezaji hao wote leo walionyesha soka safi, Simba ikicheza na Faru, Uwanja wa Kinesi. Katika mchezo huo, Simba ilitangulia kupata bao lililofungwa na Albert Malale dakika ya nne, kabla ya Mussa Pablo kuisawazishia Faru dakika ya 26.
Huku mchezo huo ukiendelea, wanachama na wapenzi wa klabu hiyo walipata fursa ya kupiga picha na Kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu.
0 comments:
Post a Comment