Wachezaji wa Ujerumani wakiwasili Poland |
UJERUMANI
|
KUNDI A
|
|
KIKOSI cha Ujerumani kimewasili Poland siku nne kabla ya kuanza kwa mechi za Euro 2012.
Watoto wa Joachim Low walitua na ndege aina ya Boeing 747, wakitokea Frankfurt majira ya saa 6:35 (GMT) mjini Gdansk, ambako timu hiyo itaweka kambi yao kwa ajili ya michuano hiyo.
Baada ya kuingia hotelini, Ujerumani walifanya mazoezi yao ya kwanza Poland katika Uwanja wa wenye uwezo wa kuingiza watazamani 10,000.
Wachezaji wote 23 walishiriki mazoezi hayo, akiwemo Bastian Schweinsteiger, ambaye amekuwa majeruhi kwa siku za karibuni.
Nyota huyo wa Bayern Munich sasa atacheza mechi ya kwanza ya Ujerumani kwenye Euro 2012 dhidi ya Ureno Jumamosi.
0 comments:
Post a Comment