• HABARI MPYA

    Monday, June 11, 2012

    WACHEZAJI TAIFA STARS WAPEWA MILIONI 15 BAADA KUUA NGE JANA-


    Kikosi cha jana

    MECHI ya mchujo ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Gambia (The Scorpions) iliyochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 124,038,000.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba mapato hayo yametokana na washabiki 31,122 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Washabiki 25,901 walikata tiketi za sh. 3,000.
    Amesema asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 18,921,050.85 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 6,555,000), bonasi kwa Taifa Stars (sh. 15,767,542.37), waamuzi (sh. 13,372,000), usafi na ulinzi (sh. 2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000), umeme (sh. 300,000) na mafuta ya jenereta (sh. 200,000).
    Amesema kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 12,834,481, asilimia 10 ya uwanja sh. 6,417,241, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 3,208,620, asilimia 20 ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 12,834,481 na asilimia 45 ya TFF (sh. 28,877,583).
     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WACHEZAJI TAIFA STARS WAPEWA MILIONI 15 BAADA KUUA NGE JANA- Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top