IMEWEKWA OKTOBA 3, 2013 SAA 3:40 USIKU
MABAO ya kipindi cha kwanza ya Jermain Defoe dakika ya 34 na Nacer Chadli dakika ya 39 yametosha kuipa ushindi wa 2-0 Tottenham katika Europa League usiku huu dhidi ya Anzhi Makhachkala nchini Urusi.
Andre Villas-Boas aliwapumzisha wachezaji wake kadhaa wa kikosi cha kwanza katika mechi hiyo, lakini mabao mawili ndani ya dakika tano yalimpa faraja dhidi ya timu ya zamani ya Samuel Eto'o aliye Chelsea kwa sasa.
Ikitoka kuifunga Tromso 3-0 katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi K, Spurs sasa imetimiza pointi sita na haijaruhusu nyavu zake kuguswa hata mara moja katika michuano hiyo.
La kwanza: Jermain Defoe (katikati) akipongezwa nawenzake baada ya kuifungia Tottenham bao la kwanza
Kikosi cha Spurs kilikuwa: Lloris, Walker, Kaboul/Dawson dk71, Chiriches, Fryers, Holtby/Eriksen dk78, Dembele, Chadli, Sandro, Lamela/Sigurdsson dk72 na Defoe.
Anzhi: Pomazan, Angbwa/Gadzhibekov dk79, Tagirbekov, Adeleye, Ewerton, Jucilei, Ahmedov, Razak, Solomatin, Serderov/Yeschenko dk56 na Abdulavov/Traore dk45.
Sapoti ya nguvu: Mashabiki wa Spurs wakiishangilia timu yao nchini Urusi