IMEWEKWA OKTOBA 4, 2013 SAA 10:43 USIKU
KLABU ya Swansea City imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya Europa League ikitoka kuifunga Valencia katika mchezo wa kwanza na usiku huu imeichapa bao 1-0 St Gallen Uwanja wa Liberty.
Bao pekee lililompa faraja kocha Michael Laudrup lilifungwa na Wayne Routledge dakika ya 52 ya mchezo huo na sasa timu hiyo inayosifika kwa kucheza soka safi ya kitabuni imefikisha pointi sita.
Kipa wa Swansea, Gerhard Tremmel alifanya kazi nzuri baada ya kuokoa mkwaju wa penalti wa mchezaji wa St Gallen, Goran Kranovic na kuzilinda pointi tatu timu yake.
Kikosi cha Swansea kilikuwa: Tremmel, Tiendalli, Flores, Amat, Davies/Dyer dk62, Britton, De Guzman, Pozuelo/Shelvey dk83, Michu, Routledge na Bony/Vazquez.
St Gallen: Lopar, Martic, Montandon/Russo dk73, Besle, Lenjani, Mutsch, Janjatovic,Vitkieviez, Mathys, Rodriguez/Nater dk62 na Karanovic/Keita dk46.
La ushindi: Wayne Routledge iifungia Swansea bao pekee katika ushindi wa 1-0 Uwanja wa Liberty
Kazi nzuri: Kipa wa Swansea, Gerhard Tremmel akiokoa penalti ya mchezaji wa St Gallen, Goran Kranovic
Nayo Wigan iling'ara kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Maribor Uwanja wa DW yaliyotiwa kimiani na Powell dakika ya 22 na 90 na Watson dakika ya 33, wakati bao pekee la wapinzani wao lilifungwa na Tavares dakika ya 60.
La pili: Nyota wa Wigan, Ben Watson akishangilia bao la pili