BAADA ya kukamilikkwa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya, joto liliopo ni je klabu nne za England zilizofuzu zitakutana na timu gani katika hatua ya mtoano, inayojumuisha timu 16.
Kuelekea droo hiyo Jumatatu mjini Nyon, BIN ZUBEIRY imetabiri timu ambazo zinaweza kukutana na klabu hizo za England katika michuano hiyo.
Mbwa mkali zaidi: Cristiano Ronaldo atataka kuboresha rekodi yake ya mabao aliyoanza nayo katika hatua ya makundi akiwa Real Madrid
Baada ya kuangukia katika nafasi ya pili kufuatia kipigo cha Napoli jana katika mchezo wa mwisho, Arsenal sasa inatarajiwa kuangukia kwa mpinzani mgumu kwenye hatua hiyo ya mtoano.
Droo huwa inazingatia mambo kadhaa kama timu kutokutana na mpinzani iliyokuwa naye kundi moja na pia timu za nchi moja kutokutanishwa, huku timu zilizoongoza makundi zikicheza mechi za marudiano za mtoano nyumbani.
Hiyo inamaanisha hakuna klabu za Ligi Kuu ya England zinazoweza kupambanishwa, lakini iko wazi The Gunners na Manchester City watakutana na wapinzani wagumu baada ya kushika nafasi za pili kwenye makundi yao.
Anapambana kuwa fiti: Lionel Messi atarajea kutoka kwenye majeruhi kuiongoza Barcelona katika hatua ya mtoano
Timu zote zinatazamiwa kutoepuka kukutana na vifofo wa Hispania, Real Madrid na Barcelona, wakati timu ya Arsene Wenger inaweza kukutana na mabingwa watetezi, Bayern Munich - City haiwezi kukutana na Bayern lakini inaweza kukutana na washindi wa pili wa msimu uliopita, Borussia Dortmund.
Kwa Chelsea na Manchester United - ratiba ngumu kwao itakuwa ni kukutana na AC Milan. Pamoja na hayo, timu mbili zilizoongoza makundi zitapata timu hafifu kidogo katika hatua ya mtoano.
ARSENAL
Real Madrid
PSG
Bayern Munich
Atletico Madrid
Barcelona
PSG
Bayern Munich
Atletico Madrid
Barcelona
CHELSEA
Bayer Leverkusen
Galatsaray
Olympiakos
Zenit St Petersburg
AC Milan
Galatsaray
Olympiakos
Zenit St Petersburg
AC Milan
MANCHESTER CITY
Real Madrid
PSG
Dortmund
Atletico Madrid
Barcelona
PSG
Dortmund
Atletico Madrid
Barcelona
MANCHESTER UNITED
Galatasaray
Olympiakos
Schalke
Zenit St Petersburg
AC Milan
Olympiakos
Schalke
Zenit St Petersburg
AC Milan



.png)
0 comments:
Post a Comment