MABASI ya timu za Paris Saint-Germain na Lyon za Ufaransa yote yalishambuliwa kwa mawe kabla ya mechi baina yao ya Ligue 1 Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris jana jioni.
Mabingwa PSG wamethibitisdha basi lao kushambuliwa na na kupasuliwa vioo wakati wakielekea uwanjani. Basi la Lyon inaaminika pia kupigwa mawe.
Baada ya chaneli ya TV ya Ufaransa, Canal + kuonyesha picha za basi la PSG lilivyoathirika, ofisa mmoja akaiambia AFP: "Basi lilipigwa mawe na kioo cha mbele kulia kilipasuka.'
Zlatan Ibrahimovic na wachezaji wenzake wa PSG wakipasha misuli moto baada ya kushuka kwenye basi lao lililopigwa mawe wakielekea Parc des Princes
Nyota wakiwemo Zlatan Ibrahimovic, Thiago Silva na Edison Cavani inaaminika walikuwamo kwenye basi hilo wakisafiri na PSG, lakini wote walikuwemo kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Laurent Blanc kilichowafumua wenyeji 4-0.
Cavani alifunga bao la kwanza kwa kichwa akiunganisha kona ya Lucas Moura dakika ya 36, kabla ya Ibrahimovic kufunga kwa penalti dakika ya 41.
Silva akafunga la tatu dakika ya 60 na Ibrahimovic akahitimisha karamu ya mabao kwa penalti tena dakika ya 83.
Edison Cavani akipiga mpira kikaretika
Mchezaji wa Lyon, Yoann Gourcuff (kulia) akiwatoka wachezaji wa PSG, Alex (kushoto) na Marco Verratti (katikati)
Mtu wa nguvu: Ibrahimovic akishangilia baada ya kufunga penalti ya kwanza dhidi ya Lyon
Tukio hilo lilitokea jirani na Chaville, linakuja kiasi cha wiki moja baada ya mashabiki wa Saint-Etienne kutolewa nje ya Uwanja wa Nice, Allianz Riviera baada ya watu wanane kujeruhiwa wakati wa mapambano baina ya mashabiki wa timu hizo.
Mashabiki wa The Greens tangu wakati huo wamefungiwa kuingia kwenye mechi za ugenini kwa kipindi chote kilichobaki cha mwaka.
0 comments:
Post a Comment