KLABU ya Barcelona imepoteza mechi ya pili mfululizo ikicheza bila nyota wake Lionel Messi aliye majeruhi, baada ya kufungwa na Athletic Bilbao 1-0 jana Uwanja wa San Mames, bao pekee la Iker Muniain dakika ya 70.
Neymar alitarajiwa kwa mara nyingine kuziba vyema pengo la Messi katika ufungaji, lakini hakufanya lolote kutokana na kuchezewa kindava na mabeki wa Bilbao.
Mshambuliaji wa Barca, Neymar alikuwa anachezewa rafu sana jana
Athletic Bilbao wakishangilia bao lao lililofungwa na Iker Muniain (wa pili kushoto)
0 comments:
Post a Comment