Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
MSHAMBULIAJI Thomas Emanuel Ulimwengu jana ametua mjini Nairobi, Kenya kukiongezea nguvu kikosi cha Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki Kati, CECAFA Challenge mwenzake Mbwana Ally Samatta atawasili leo jioni.
Stars imeambulia pointi nne na mabao mawili baada ya mechi mbili za Kundi kwa sare ya 1-1 na Zambia katika mchezo wa kwanza na ushindi wa 1-0 dhidi ya timu dhaifu, Somalia jana.
Wawili hao wanawasili wakitoka kuichezea timu yao, TP Mazembe ya DRC katika Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambayo walifungwa jumla ya mabao 3-2 na kukosa Kombe.
Tout Puissant Mazembe ilishinda 2-1 dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia, katika fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, hivyo kuangushwa kwa matokeo ya jumla ya 3-2, baada ya awali kufungwa 2-0 Uwanja Olympique de Rades mjini Tunis katika Fainali ya kwanza.
Mazembe ilitakiwa kushinda mabao 3-0 Jumamosi nyumbani ili kutwaa taji hilo, na ilionekana kama ingeweza kufanya hivyo baada ya kuongoza kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 88, yaliyofungwa na nyota wa Mali, Traore Cheibane dakika ya 10 na Samatta dakika ya 24.
Lakini wakati Mazembe wakiwa bize na mashambulizi ya kusaka bao la tatu dakika za lala salama, Ben Youssef akaifungia bao muhimu Sfaxien dakika ya 88 na kuzima ndoto za akina Samatta kuvaa Medali za Dhahabu za Kombe la Shirikisho.
Katika mchezo wa kwanza, mabao yaliyoizamisha Mazembe yalifungwa na washambuliaji wa kimataifa wa Gabon, Ibrahim Didier Ndong aliyefunga bao la kwanza dakika ya 16 na mshambuliaji Taha Yassine Khenissi aliyefunga la pili dakika ya 90 na ushei wakimtungua kipa mahiri, Robert Muteba Kidiaba.
Washambuliaji wote wa Tanzania, Samatta na Ulimwengu walianza katika kikosi cha Mazembe pamoja na Tressor Mputu Mabi, lakini hawakuweza kuwanusuru mabingwa mara nne Afrika na kipigo hicho.
Sfaxien, timu pekee iliyoshinda Kombe la Shirikisho mara mbili tangu kutambulishwa kwa mfumo mpya mwaka 2004, yenye maskani yake katika mji uliozungukwa na bahari ya Mediterranean, Sfax kwa ushindi huo imezawadiwa kitita cha dola za Kimarekani, 625 000, wakati Mazembe wamepata dola 432 000.
Sfaxien pia watamenyana na mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, Al Ahly ya Misri kuwania taji la Super Cup mechi itakayopigwa nchini Misri Februari 2014.

![]() |
Samatta alifunga bao moja Mazembe ikishinda 2-1 dhidi ya Sfaxien na chini ni Thomas Ulimwengu |

0 comments:
Post a Comment