• HABARI MPYA

    Monday, December 02, 2013

    ZANZIBAR KATIKA WAKATI MGUMU MNO CHALLENGE

    Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
    ZANZIBAR iko hatarini kuwakosa wachezaji wawili tegemeo, Nahodha Khamis Mcha ‘Vialli’ na Suleiman Kassim ‘Selembe’ katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi A, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na kati, CECAFA Challenge dhidi ya wenyeji, Kenya kesho kutokana na kuwa majeruhi. 
    Majeruhi; Suleiman Kassim 'Selembe' akiwa benchi juzi baada ya kuumia dhidi ya Ethiopia

    Viungo hao wawili hao wote wanasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja na Vialli hakucheza kabisa mchezo uliopita dhidi ya Ethiopia, wakati Selembe alitoka ndani ya robo saa kumpisha Seif Abdallah Karihe baada ya kuumia.
    Wazi huu ni mtihani mzito kwa Zanzibar, ambayo inatakiwa kushinda kesho ili kujihakikishia kuingia Robo Fainali, au kwa matokeo mengine, isubiri kubahatisha kuingia kama ‘best looser’.
    Sudan Kusini itaanza na Ethiopia mchana kabla ya Kenya kumalizana na Zanzibar jioni. Ethiopia na Kenya zina pointi sawa nne kila moja, wakati Zanzibar ina pointi tatu na Sudan Kusini ambayo haina pointi inashika mkia.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZANZIBAR KATIKA WAKATI MGUMU MNO CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top