• HABARI MPYA

    Sunday, December 01, 2013

    WASOMALI WALIVYOITOA JASHO STARS LEO NYAYO

    Mshambuliaji wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Mrisho Ngassa kushoto akimtoka beki wa Somalia katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mchana wa leo, Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya. Bara ilishinda 1-0.

    Mfungaji wa bao pekee la Stars, Haroun Chanongo akimtoka beki wa Somalia, Mohamed Tahlil Shidane

    Nahodha wa Somalia, Hassan Ali  Roble akiteleza kuondosha mpira miguuni mwa Amri Kiemba wa Stars

    Hassan Ali Roble akimdhibiti Erasto Nyoni wa Stars

    Mshambuliaji wa Stars, Elias Maguri akiwatoka mabeki wa Somalia

    Mrisho Ngassa akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa Somalia

    Beki wa Somalia akibinuka tik tak nyuma ya Elias Maguri wa Stars

    Kiungo wa Stars, Salum Abubakar 'Sure Boy' akipambana na kiungo wa Somalia, Sidi Mohamed Omer

    Haroun Chanongo akimpiga tobo beki wa Somalia, Aden Hussein Ibrahim

    Ramadhani Singano 'Messi' akimtoka beki wa Somalia anayepambana hadi kuanguka chini 

    11 wa Stars walioanza leo

    Wasomali walioitoa jasho Stars

    Benchi la Stars wakati wa wimbo wa Taifa

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WASOMALI WALIVYOITOA JASHO STARS LEO NYAYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top