• HABARI MPYA

    Wednesday, November 19, 2014

    NIGERIA WAVULIWA UBINGWA AFRIKA, WALAZIMISHWA SARE 2-2 NA BAFANA BAFANA NYUMBANI

    MABINGWA wa Afrika, Nigeria leo wametema rasmi taji baada ya kushindwa kufuzu kwenye Fainali zijazo za Mataifa ya Afrika kufuatia kulazimishwa sare ya 2-2 nyumbani na Afrika Kusini katika mchezo wa Kundi A.
    Bafana Bafana imeifanyia 'roho mbaya' tu Nigeria kwani ilikuwa imekwishafuzu na katika mchezo wa leo, iliongoza muda mrefu kwa mabao 2-0 kabla ya wenyeji kusawazisha dakika za mwishoni.
    Nigeria sasa haitakwenda Equatorial Guinea Januari mwakani kutetea taji lao, baada ya Kongo kuilaza 1-0 Sudan mjini Kharotum na kuungana na Bafana kwenda AFCON, huku Super Eagles ikimaliza katika nafasi ya tatu.
    Mabingwa wa Afrika, Nigeria wametemeshwa taji mapema leo 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NIGERIA WAVULIWA UBINGWA AFRIKA, WALAZIMISHWA SARE 2-2 NA BAFANA BAFANA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top