• HABARI MPYA

    Monday, May 18, 2015

    FALCAO, DE GEA WAWAPA MIKONO YA KWAHERI MANA UNITED

    MSHAMBULIAJI Radamel Falcao amewaaga mashabiki wa Manchester United baada ya kutolewa jana katika mchezo dhidi ya Arsenal dalili ambazo zinaonyesha nyota huyo wa Colombian hatabaki Old Trafford anakocheza kwa mkopo.
    Umekuwa msimu mgumu Manchester kwa Falcao baada ya kutua kwa mkopo kutoka Monaco mwaka jana na inaonekana muda wake wa kuwa Old Trafford utafikia mwisho.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alimpisha Robin van Persie baada ya saa moja katika sare ya 1-1 na Arsenal, na wakati anaondoka uwanjani, aliwapungia mkono wa kwaheri mashabiki wa kona zote Old Trafford kama anawaaga.
    Radamel Falcao waved goodbye to Manchester United fans during the draw with Arsenal on Sunday
    Radamel Falcao akiwapungia mkono wa kwaheri mashabiki wa Manchester United jana katuika mechi na Arsenal jana

    Tukio hilo lilikumbushia mwaka 2009 wakati Carlos Tevez alipojua ataondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu huo akawapungia mkono mashabiki Manchester United.
    United itatakiwa kuilipa Monaco Pauni Milioni 46 ili kumbeba jumla Falcao kutoka Mkataba wa sasa wa mkopo, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amefunga mabao manne tu msimu mzima katika mashindano yote.
    Mcolombia huyo alianza kuwika katika ulimwengu wa soka wakati anachezea Atletico Madrid ya Hispania, lakini baada ya kuumia mguu katika msimu wake wa kwanza, Monaco akaondolewa katika kikosi cha Kombe la Dunia mwaka jana.
    Falcao was replaced on the hour mark by Robin van Persie
    Falcao was replaced on the hour mark by Robin van Persie
    Falcao alimpisha Robin van Persie (kulia), katika mchezo wa jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    TAKWMU ZA MSIMU ZA RADAMEL FALCAO

    Mechi alizocheza: 26
    Mabao: 4
    Mashuti: 29
    Pasi za mabao: 4 
    Kadi ya njano : 2 
    Chanzi: www.premierleague.com 
    Katika mwaka wake wa kwanza Old Trafford, Falcao ameonekana kama samaki aliyetolewa majini na amekuwa akicheza kama msaidizi wa Wayne Rooney na Robin van Persie.
    Kipa David de Gea pia alitolewa jana baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Mspanyola nwenzake, Victor Valdes dakika 15 za mwisho.
    Naye staili yake ya kuagana na mshabiki wakati anatoka inaongeza wasiwasi kwamba arahamia Real Madrid, ambao wanamtaka mno arejee kufanya kazi nyumbani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FALCAO, DE GEA WAWAPA MIKONO YA KWAHERI MANA UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top