KIUNGO wa Ghana, Harrison Afful alikuwa katika kiwango kizuri jana na kuisaidia Esperance kuifumua Hearts of Oak mabao 4-0 katika mechi ya mchujo kuwania kucheza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.
Mshambuliaji wa Nigeria, Samuel Eduok alifunga bao la kwanza dakika ya 11 kabla ya kutengenezewa bonge la pasi na Afful kufunga bao lake la pili katika mchezo huo dakika ya 57. Afful akafunga yeye mwenyewe kwa shuti la kubabatiza dakika ya 73, lakini hakushangilia kwa sababu Hearts of Oak ni ya nyumbani Ghana.
Dakika sita baadaye, Ghaylane Chaalali akakamilisha sherehe za mabao za Esperance mjini Tunis katika mchezo huo wa kwanza wa kuwania kuingia kwenye makundi ya Kombe la Shirikisho.
Hearts of Oak sasa itatakiwa kushinda 5-0 nyumbani ili kuwatoa Watunisia hao katika mchezo wa marudiano Uwanja wa Accra Juni 7.
Katika mechi nyingine za kwanza za hatua hiyo jana Al Ahly imeifunga 2-1 Club Africain,
Sanga Balende imeilaza 1-0 Zamalek, AC Leopards imeifunga 3 – 0 Warri Wolves, wakati juzi Sfaxien imeifunga 2 – 0 ASEC Mimosas, Raja Casablanca imeichapa 2 – 0 Etoile du Sahel, Stade Malien imeilaza 2-0 AS Vita na Ijumaa AS Kaloum ilifungwa nyumbani 2-0 na Orlando Pirates mjini
Bamako.

![]() |
| Harrison Afful (kushoto) jana alikuwa mwiba kwa timu ya nyumbani kwao, Hearts Of Oak |
Hearts of Oak sasa itatakiwa kushinda 5-0 nyumbani ili kuwatoa Watunisia hao katika mchezo wa marudiano Uwanja wa Accra Juni 7.
Katika mechi nyingine za kwanza za hatua hiyo jana Al Ahly imeifunga 2-1 Club Africain,
Sanga Balende imeilaza 1-0 Zamalek, AC Leopards imeifunga 3 – 0 Warri Wolves, wakati juzi Sfaxien imeifunga 2 – 0 ASEC Mimosas, Raja Casablanca imeichapa 2 – 0 Etoile du Sahel, Stade Malien imeilaza 2-0 AS Vita na Ijumaa AS Kaloum ilifungwa nyumbani 2-0 na Orlando Pirates mjini
Bamako.

.png)
0 comments:
Post a Comment