• HABARI MPYA

    Monday, May 18, 2015

    TIMU YA NGASSA YANG’ARA TUZO ZA LIGI KUU AFRIKA KUSINI, KOCHA WA ZAMANI YANGA ‘ALA ZA USO’

    Na Mwandishi Wetu, JOHANNESBURG
    TIMU mpya ya Mrisho Khalfan Ngassa, Free State Stars imetoa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini, ambaye ni Moeketsi Sekola. Ngassa amejiunga na FS mwezi huu kama mchezaji huru, akitokea Yanga SC ya nyumbani kwao, Tanzania.
    Lakini ni beki wa Kaizer Chiefs, Tefu Mashamaite aliyefunika katika tuzo za msimu Ligi Kuu ya Afrika Kusini, maarufu kama PSL katika sherehe zilizofanyika ukumbi wa Sandton Convention Centre mjini Johannesburg, Afrika Kusini usiku wa jana.
    Mashamaite ameshinda tuzo tatu kati ya nne alizokuwa anawania, huko kocha wa zamani wa Yanga SC, Mserbia Kostadin Papic anayeifundisha Polokwane City FC akitoka kapa. 
    Mrisho Ngassa kushoto amejiunga na Free State Stars ambayo imetoa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini 

    Beki wa ‘The Amakhosi’ aliondoka na tuzo za Mwanasoka Bora wa msimu wa 2014/2015, Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya ABSA wa Msimu na beki bora wa Ligi Kuu wa msimu ya ABSA. Kwa ujumla, Mashamaite ameondoka na kitita cha randi 450 000.
    Kiungo wa Mamelodi Sundowns, Teko Modise ameshinda tuzo ya kiungo bora wa msimu akiondoka na Randi 50, 000 na akapata pia Randi 150,000 kwa kuwa mchezaji bora wa Kombe la Nedbank.
    Mchezaji wa SuperSport United, Dove Wome ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mashindano ya mtoano ya Telkom na kupata Randi 200,000, wakati George Maluleka wa while Kaizer Chief ameshinda tuzo ya MTN8 na kupata Randi 80,000.
    Moeketsi Sekola wa Free State Stars ndiye mkali wa mabao Afrika Kusini

    WASHINDI WA TUZO ZA MSIMU AFRIKA KUSINI
    MCHEZAJI BORA WA MSIMU: Randi 250, 000
    Tefu Mashamaite (Kaizer Chiefs) – MSHINDI
    TUZO YA MWENYEKITI
    Botha Smila
    LIGI KUU YA ABSA
    Mchezaji Bora wa Msimu – Randi 150, 000
    Tefu Mashamaite (Kaizer Chiefs) – MSHINDI 
    (Pamoja na Randi 10,000 iwapo mshindi ana akaunti katika benki ya ABSA)
    Kipa Bora wa Msimu Ligi Kuu ya ABSA– Randi 50,000
    Moeneeb Joseph (Bidvest Wits) - MSHINDI
    (Pamoja na Randi 10,000 iwapo mshindi ana akaunti katika benki ya ABSA)
    Beki Bora wa Msimu Ligi Kuu ya ABSA– R50 000
    Tefu Mashamaite (Kaizer Chiefs) - MSHINDI
    (Pamoja na Randi 10,000 iwapo mshindi ana akaunti katika benki ya ABSA)
    Kiungo Bora wa Msimu Ligi Kuu ya ABSA – Randi 50,000
    Teko Modise (Mamelodi Sundowns) - MSHINDI
    (Pamoja na Randi 10,000 iwapo mshindi ana akaunti katika benki ya ABSA)
    Mchezaji Bora Chipukizi wa Ligi Kuu ya ABSA– Randi 50,000
    Phumlani Ntshangase (Bidvest Wits) - MSHINDI
    (Pamoja na Randi 10,000 iwapo mshindi ana akaunti katika benki ya ABSA)
    Kocha Bora wa Msimu wa Ligi Kuu ya ABSA – Randi 75,000
    Stuart Baxter (Kaizer Chiefs) – MSHINDI 
    (Pamoja na Randi 10,000 iwapo mshindi ana akaunti katika benki ya ABSA)
    Bao Bora la Msimu Kuu ya ABSA– Randi 50 000
    Menzi Masuku (Orlando Pirates) – MSHINDI 
    (Mechi namba 54, Orlando Pirates vs SuperSport United –Aprili 29, mwaka 2015) 
    (Pamoja na Randi 10,000 iwapo mshindi ana akaunti katika benki ya ABSA)
    Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya ABSA– Randi 25 000
    Moeketsi Sekola (Free State Stars) 
    (Pamoja na Randi 10,000 iwapo mshindi ana akaunti katika benki ya ABSA)
    Beki wa Kaizer Chiefs, Tefu Mashamaite (kulia) akipokea tuzo yake usiku wa jana kutoka kwa mwanasoka wa zamani wa kimataifa wa Afrika Kusini, Lucas Radebe (kushoto) 

    KOMBE LA NEDBANK
    Mchezaji Bora wa Kombe la Nedbank: Randi 150, 000 
    Teko Modise (Mamelodi Sundowns) - MSHINDI
    Mchezaji Bora Anayechipukia Kombe la Nedbank: Randi 50,000
    Tashreeq Morris (Ajax Cape Town) – MSHINDI
    MICHUANO YA MTOANO YA TELKOM
    Mchezaji Bora wa Telkom: Randi 200,000
    Dove Wome (SuperSport United) – MSHINDI
    Michuano ya MTN8
    Mchezaji Bora wa MTN8: Randi 80,000 
    George Maluleka (Kaizer Chiefs) – MSHINDI
    LIGI YA TAIFA DARAJA LA KWANZA
    Mfungaji bora wa Msimu: Randi 50,000 
    Phumelele Bhengu (Thanda Royal Zulu)
    MICHUANO YA MULTICHOICE DISKI;
    Mchezaji Bora wa mashindano
    Dikgang Ngcobo
    TUZO ZA MAREFA:
    Refa Bora wa Msimu: Randi 50,000
    Shumani Phillip Tinyani – MSHINDI
    Mshika Kibendera Bora wa Msimu: Randi 40,000 
    Peter Chauke – MSHINDI
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TIMU YA NGASSA YANG’ARA TUZO ZA LIGI KUU AFRIKA KUSINI, KOCHA WA ZAMANI YANGA ‘ALA ZA USO’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top