BONDIA Floyd 'Mtu Pesa' Mayweather ameendelea kutengeneza fedha hata anapokuwa nje ya ulingo, baada ya mbabe huyo mwenye umri wa miaka 38 kuposti kwenye akaunti yake ya Instagram juu ya kushinda kamari.
Katika kamari alizocheza kwenye mchezo wa mpira wa kikapu na pambano la baina ya Gennady Golovkin na Willy Monroe, Mayweather ametengeneza jumla ya dola za Kimarekani 827, 272.73 kutoka mtaji wa dola 350, 000 alizoweka.
Anapata fedha hizo akitoka kushinda pambano la utajiri mkubwa na la karne, dhidi ya Manny Pacquiao mapema mwezi huu.
Floyd Mayweather akishuhudia mchezo wa NBA LA Clippers na Houston Rockets
Floyd 'Mtu Pesa' Mayweather ameposti juu ya kamari alizoshinda katika akaunti yake ya Instagram
Mayweather alipigana kwa tahadhari kubwa dhidi ya mpinzani mwenye mikono mizito, Pacquiao ukumbi wa MGM Grand Garden Arena Mei 2, mwaka huu na kushinda kwa pointi hivyo kufanikiwa kuunganisha taji la WBO uzito wa Welter duniani pamoja na matajoi ya WBC na WBA.
Bondia ambaye hajawahi kupoteza pambano, alimshinda Mfilipino huyo kwa pointi za majaji wote 118-110, 116-112 na 116-112.
Tangu aanze kupigana ngumi za kifua wazi, Mayweather amepanda ulingoni mara 48 na kushinda mapambano yote, kati ya hayo, 26 akishinda kwa Knockout (KO).
Mayweather alimtabiria Gennady Golovkin (kushoto) atampiga Willie Monroe Jr mapema wiki hiii


.png)
0 comments:
Post a Comment