Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
Unaposikia `neno` `uswahili` ingawa siyo tafsiri halisi ama iliyopitishwa inamaanisha kufanya jambo `kiujanja ujanja` bila kupitia misingi inayotakiwa.
Mtu anapokwambia acha `uswahili bwana` moja kwa moja unaelewa amemaanisha acha `ujanja ujanja au kutokufanya jambo kiusahihi, udanganyifu au kuhadaa jambo Fulani`.
Francis Kaswahili ni rafiki yangu sana, mara nyingi hupenda kuvaa `majoho` kama wanayovaa watu wengi wa nchini Nigeria na kofia juu maarufu kama `kibandiko`.
Nakumbuka siku moja tulikuwa katika Makaburi ya Kisutu tukishiriki kumzika mmoja kati ya wanamuziki `nguli` wa Nchini, nilikuwa na Kaswahili akiwa amevaa `joho` la Njano na kofia juu.
Mara kwa mara Kaswahili hubeba mkoba wake mweusi na joho lake basi anapendeza sana ukimkuta huko `mijini`.
Ingawa sifahamu ndani ya Begi kahifadhi kitu gani lakini huwa anapendeza sana.
Mimi namheshimu sana Mkubwa wangu Kaswahili na nitaendelea kumuheshimu kwa kuwa naamini hata yeye ananiheshimu (kama anasoma hapa najua atakuwa anatabasam na kutikisa kichwa akiashiria kukubaliana nami).
Hivi Karibuni `rafiki yangu` Kaswahili akaibua `kituko` kipya ambacho sasa kitamlazimu asimame kujibu na kujitetea ili kurejesha heshima yake (imetetereka).
Kaswahili `alikurupuka`akatangaza tarehe ya Uchaguzi wa timu ya Yanga na bei ya kununua Fomu na taratibu zote alizokuja nazo.
Ni kweli kuwa ``rafiki yangu` Kaswahili alikuwa katika Kamati ya uchaguzi iliyopita ya Yanga SC iliyomuweka madarakani, Mwenyekiti wa sasa wa Yanga ( RAIS?)
Lakini Kamati hiyo iliyokuwa chini ya Mwenyekiti, Jaji John Mkwawa, Makamu Ridhiwani Kikwete, Katibu Kaswahili na Wajumbe Yusuph Mzimba na Philemon Ntahilaja ilishavunjwa muda mrefu.
Lakini Rafiki yangu huyu aliibuka majuzi hapa akatangaza utaratibu wote lakini eneo litakapofanyika uchaguzi akasema itatangazwa baadae.
Wakati Kaswahili anayafanza hayo, kule Burundi nako kulikuwa na hali tete baada ya Jenerali wa Jeshi la nchi hiyo, Godefroid Niyombare kutaka kumpindua Rais na mwanasoka wa zamani wa taifa hilo, Pierre Nkurunzinza wakati akiwa kwenye Mkutano Tanzania.
Bahati nzuri, zoezi hilo liliitikisa tu Burundi, lakini mapinduzi hayakufanikiwa. Huenda waliyotekeleza hayo watashitakiwa kwa makosa ya `uhaini`.
Kama rafiki yangu Kaswahili angeyafanya haya huko katika Siasa leo angekuwa kizimbani kwa kesi ya uhaini.
Kama Kaswahili alikuwa anafahamu Kamati yake ilishavunjwa kwa nini akaibuka na `joho` lake kutangaza uchaguzi?
Ina maana hakuwa na taarifa za kuvunjwa kamati yake ya uchaguzi na sasa Mwenyekiti wake ni Mwanasheria Alex Mgongolwa?
`Majoho` yote yale na begi akose taarifa hizo? Kaswahili alikaa na kamati gani akatangaza tarehe ya Uchaguzi? Alipanga bei ya Fomu kwa kutumia vigezo gani?
Alipata Baraka wapi?
Kaswahili alilipia kadi yake ya uanachama Yanga mara ya mwisho lini? Ni mwanachama hai? Alikuwa na vigezo kutangaza uchaguzi? Kama yeye ni katibu ni nani Mwenyekiti wake? Walikaa kikao lini na wapi? Muhtasari uko wapi? Alikuwa anataka kufanya Mapinduzi kama Burundi?
Katiba ya Yanga inasemaje katika suala la Uchaguzi?
Angepeleka wapi Fedha alizouzia Fomu?
Ni maswali ambayo unaweza usiwe na majibu lakini majibu yote anayo Franciss Kaswahili na akijibu hayo basi atakua amejivua `joho` la kashfa linalomwandama kwasasa.
Kaswahili ni rafiki yangu sana na nina maswali mengi sana ya kumuuliza na anipe majibu sahihi ili kunisogeza jirani na ukweli anaoamini yeye kwakuwa mpaka sasa nipo mbali na ukweli anaoamini yeye.
Mara baada ya kupata taarifa hizi nilimpigia simu lakini kwa bahati mbaya hakupatikana hewani,najua akishasoma hapa atanipigia kunipa ukweli na kunitoa gizani,vinginevyo mpaka sasa namuona kama kafanya `uswahili tu`.
(Mwandishi wa makala haya ni mtangazaji wa Redio One na ITV, ambaye anapatikana kwa namba +255 655 250157 na +255 655 250157)

.png)
0 comments:
Post a Comment