Sikumbuki ni lini Tanzania tumewahi kuwa na mwimbaji supastaa nje ya mipaka yetu kama Naseeb Abdul “Diamond” kama yupo naomba radhi kwa kumsahau.
Simaanishi kuwa hatujawahi kuwa na waimbaji wazuri wa muziki kuliko Diamond, la hasha! Wako wengi tena waliomzidi Diamond kwa mbali sana, lakini ni ukweli kuwa wengi wao walitamba zaidi katika eneo la ukanda wa Afrika Mashariki, lakini Diamond ‘ametusua’ Afrika nzima na kupenya hadi ya mipaka ya bara hili.
Diamond ameshiriki tuzo kadhaa za muziki za kimataifa, ameshirikiana na wamuziki kadhaa nyota wa Afrika, amekuwa na ushawishi wa hali ya juu kwenye soko la muziki wetu.
Amekuwa kichocheo cha wasanii wengi kutengeneza video za gharama na za kiwango cha kimataifa, ana uwezo wa kuwafanya Watanzania waanze kuamini na kuzipenda nyimbo zetu zenye vionjo vya kiasili, “Mdogo Mdogo” na “Nasema na Wewe” ni ushahidi tosha wa namna Diamond anavyoanza kuutoa muziki wa kizazi kipya kwenye ukiritimba wa kuchukua vionjo vya Kinigeria.
Kwa hali hiyo hiyo, Diamond pia ana nafasi ya kuubomoa na kuuyumbisha muziki wa nyumbani, kauli zake na nyendo zake zinaweza kuwa na athari kubwa kwa jamii kutokana na ukweli kuwa ana wafuasi na mashabiki wengi nyuma yake.
Mwaka jana Diamond alichukua tuzo saba za Kilimanjaro Tanzania Music Awards, ikiwa ni rekodi mpya katika tuzo hizo na haijulikani ni lini atapatikana msanii wa kuivunja.
Safari hii Diamond ameingi kwenye vipengele vitano vya Kili Awards ikimaanisha kuwa hana nafasi ya kufikia mafaniko ya mwaka jana.
Majuzi Diamond kupitia akaunti yake ya Instagram akatoa kauli ambayo tafsri yake ilikuwa ni moja tu – kuziponda tuzo za Kili – kwa kudai kuwa tuzo hizo kwake hazimpunguzii wala kumuongezea chochote, akataja baadhi ya wasanii ambao anaamini hawakutendewa haki, hali inayomfanya asione haja ya kuomba kura za mashabiki wake kwa vile hata bila tuzo hizo bado ataendelea kuwa juu.
Sipingani na Diamond, inawezeka kabisa kama anavyosema yeye kuwa tuzo hazimpumzii chochote, lakini hakuna ubishi kuwa zinaongeza heshima, kusema tuzo hizo hazimuongezei mtu chochote ni sawa kabisa na “Sizitaki mbichi hizi”.
Diamond huyuhuyu ambaye huwa anakwenda kwenye sherehe za tuzo za Kili kwa maandalizi makubwa, akibadilisha nguo zaidi ya mara tatu katika usiku mmoja, leo anatuambia tuzo hazina maana!? Inashangaza kidogo.
Hizi ndio tuzo kubwa na za pekee za muziki tulizonazo hapa nchini, tunapaswa kuzipa hsehima yake – hata kama kuna mapungufu yanayojitokeza mwaka hadi mwaka basi kwa aina ya msanii kama Diamond anapaswa kutumia njia ya kiungwana kuelimisha na kutoa maoni yake.
Diamond ni kioo cha wasanii wengi, kauli yake inaweza ikawayumbisha wasanii wengi hususan wale chipukizi, kama kweli tuzo zimepoteza maana kwake basi suluhisho ilikuwa ni kujitoa na si kuziponda huku ukiendelea kushiriki kimtegomtego.
Kwa miezi ya hivi karibuni Diamond amekuwa kwenye ushindani mkubwa sana na Ali Kiba, ushindani unaotegemewa kuonekana zaidi kwenye tuzo za Kili ambazo ni wazi kuwa wasanii hao wawili watakuwa kwenye vita ya kufunikana.
Kiba yupo kwenye vipengele sita na tayari mashabiki wa muziki wanaamini kuwa kauli ya Diamond ni hatua yake ya kwanza katika kujihami na ushindani dhidi ya Ali Kiba katika tuzo hizo ili hata akifunikwa basi ionekane alishazipuuza tangu mwanzo …”Sizitaki mbichi hizi”.
Namheshimu sana Diamond kwa mafanikio yake mengi, nilizidi kumheshimu na kumpenda pale alimpozawadia gari mwanamuziki mkongwe marehemu Muhidi Maalim Gurumo, kwangu mimi Diamond ni Michael Jackson wetu Tanzania, lakini ni vema akawa makini kuchagua cha kuongea. Tuzipe heshima yake tuzo za Kili.

.png)
0 comments:
Post a Comment