KWELI NI MPIRA WA MIGUU, LAKINI SI KWA MATEKE HAYA!
Wachezaji wa Azam FC, beki Mghana Daniel Amoah (kulia) na kiungo Mcameroon Stephan Kingue (kushoto) walijikuta wakichezeana rafu wenyewe juzi Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika harakati za kumdhibiti kiungo wa Simba, Muzamil Yassin (katikati) katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC). Simba ilishinda 1-0
Wachezaji wa kigeni wa Azam wanapeana maumivu huku kiungo wa Simba akijitoa
Tukio lilianzia hapa, wakati Muzamil Yassin anajivuta kupiga mpira
Baadaye, aliyeonekana kuugulia zaidi maumivu ni Kingue
0 comments:
Post a Comment