KIKOSI cha Simba, chini ya kocha mpya, Mserbia Zoran Manojilovic ‘Maki’ kinaendelea na mazoezi katika kambi yake ya Ismailia nchini Misri kujiandaa na msimu mpya. Simba imeondoka na wachezaji wake wote, wakiwemo wapya, wazawa wawili, kiungo Nassoro Kapama kutoka Kagera Sugar na mshambuliaji Habib Kyombo kutoka Mbeya Kwanza iliyoshuka Daraja. Wengine ni wageni kiungo Mnigeria, Victor Akpan kutoka Coastal Union, winga Mghana, Augustine Okrah kutoka Asante Kotoko ya kwao na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri kutoka Zanaco ya kwao na kitarejea nchini Agosti 5 kwa ajili ta Tamasha lake la Simba Day siku tatu baadaye.
0 comments:
Post a Comment